Thursday, January 20, 2011

Makumbusho ya Taifa ya Majimaji yana mengi ya kuvutia

Vivutio vya utalii makumbusho ya Taifa ya Majimaji vyamstaajabisha  Rais wa Zanzibar
-Asema yana mambo muhimu ya kujivunia
Na Albano Midelo.

Makumbusho ya taifa ya Majimaji yaliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma ambayo yamepandishwa hadi  mapema mwaka huu tayari yamekuwa ni moja na vivutio vikubwa vya utalii wa kiutamaduni na kihistoria kutokana na viongozi wa juu wa serikali kuanza kutembelea makumbusho hayo.

Viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wanapofanya ziara  katika mkoa wa Ruvuma ,kabla ya kumaliza ziara zao wanahakikisha kuwa wanafanya ziara ya kutembelea makumbusho ya Taifa ya majimaji ambayo ndiyo makumbusho pekee nchini yenye vifaa na historia adimu katika makumbusho zote sita za kitaifa zilizomo nchini.

Miongoni mwa viongozi wakubwa wa kitaifa ambao wametembelea makumbusho hayo katika ziara zao mkoani Ruvuma ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete,Rais wa Nzanzibar Dk.All Mohamed Shein,Spika mstaafu wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania,katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Dk,Ladislaus Komba ,baadhi ya waziri,wakuu wa mikoa na wageni wengine wa ndani na nje ya nchi wakiwemo mabalozi.

 Rais wa Zanzibar Dk.Ally Mohamed Shein ametembelea makumbusho  ya Taifa ya majimaji ambapo ametoa rai kwa watanzania kuboresha sekta ya utalii  kwa kujenga tabia ya kutembelea vivutio vyote vilivyopo katika eneo husika badala ya kusubiri watalii kutoka nje ya nchi.

“Wananchi wa mkoa wa Ruvuma mmebahatika kuwa na makumbusho ya mashujaa wa vita vya majimaji,mnapopata nafasi mtembelee hapa ili kujifunza mambo mbalimbali ya historia ya vita vya majimaji pamoja na kuona vifaa halisi vilivyotumika,nimefurahi sana kufika hapa sijawahi kufika zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari na kusoma katika vitabu vya historia ya vita vya majimaji”alisema.

Dk.Shein ametembezwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo kaburi la pamoja walikozikwa mashujaa 68 walionyongwa na kuzikwa katika kaburi moja pamoja na kungalia vifaa mbalimbali vilivyotumika wakati wa harakati za ukombozi  dhidi ya mkoloni wa kijerumani   katika historia ya mtanzania wa Ruvuma ambayo ni urithi wa Taifa.
Anaongeza kuwa mahali ambapo yapo makumbusho ya vita vya majimaji panatoa nafasi ya pekee ya kukutana na kupata masimulizi ya moja kwa moja kutoka kwa wajukuu wa mashujaa waliyorithishwa kwa mapokeo kutoka kizazi kilichoshuhudia vita vya majimaji.

Ukiwa katika makumbusho ya vita vya majimaji unashuhudia kwa macho  mahali ambapo machifu na wapiganaji wa vita vya majimaji waliponyongewa hadi kufa katika awamu tofauti,pia kuna kaburi walipozikwa watu walionyongwa,kaburi hilo walichimba wenyewe kabla ya kunyongwa.

Kumbukumbu nyingine muhimu ya mashujaa wa vita vya majimaji ni kuwepo kwa kumbukumbu za shujaa mwanamke(Mkomanile) chifu ambaye ainyongwa pamoja na wanaume,ni ushuhuda muhgimu unaoonesha kwamba wanawake pia kama wanaume walishiriki katika mapambano.

Makumbusho ya mashujaa wa vita vya majimaji yanatukumbusha utamaduni wa asili ya kiafrika,hatua ya maendeleo ya ujuzi wa asili wa kiafrika na kiteknolojia iliyokuwa imefikiwa na jamii za kusni mashairiki mwa Tanzania kabla ya kuingiliwa na wakoloni ambapo jamii ziliweza kuyeyusha chuma na kutengeneza zana za chuma kama mikuki na mishale.

Inatosha kuamini kuwa kuwepo kwa silaha za mikuki na mishale kuliwapa hamasa ya ziada ya kupigana na waliweza kuendelea na mapigano kwa muda mrefu kwa kuwa hawakuwa tegemezi katika kupata silaha hizo na kwamba udhaifu wa ngao za asili katika kujikinga wasidhurikr na risasi ni miongoni mwa sababu za kutumia imani ya dawa kama kinga ambayo walidhani ingefaa katika mapambano dhidi ya wajerumani.

Matumizi ya dawa ya maji kama kinga ni kielelezo cha ubunifu wa viongozi wa jadi kuwaunganisha watu kwa kutumia imani na utamaduni wa kiafrika,hii inaonesha kuwa viongozi wa mapigano walijua nguvu kubwa ya imani kuhusu kinga na tiba za jadi.

Makumbusho ya vita vya majimaji kama yalivyo makumbusho mengine ya kihistoria ni chombo cha kuelimisha jamii kuhusu mambo muhimu ya kujivunia ya Taifa,makumbusho ya majimaji ni historia nzuri na kiburudisho pamoja na kuwa chombo cha kujenga hamasa ya kujiamini kama Taifa na kuimarisha umoja,kuheshimiana na kuishi kwa amani.

Miaka zaidi ya 100 baada ya vita vya majimaji watanzania wamejifunza mengi na kujenga upendo miongoni mwao na mahusiano mazuri na watu wa mataifa mengine,machungu ya vitan vya majimaji hayajasahauliaka,lakini utamaduni mpya umejengeka miongoni mwa watanzania wa kuheshimiana bila kujali kabila,dini rangi na sili ya mtu anakotoka.

“Huu ni ukomavu uliojengwa kihistoria tangu nchi ilipopata uhuru,makumbusho ya Taifa yanaendeleza jukumu hilo la kujenga Taifa lenye amani,kuheshimiana na umoja katika dunaia moja ya utandawazi kwa manufaa ya vizazi vyote”anasisitiza.

Kaimu mkuregenzi wa makumbusho ya Taifa  Jackson Kihiyo anasema kitendo kilichofanywa na Rais wa Zanzibar kutembelea makumbusho ya mashujaa wa vita vya majimaji ni heshima kwa mkoa wa Ruvuma pamoja na mashujaa waliozikwa katika eneo hilo kutokana na kujitolea muhanga hadi kupoteza maisha yao kwa ajili ya ukombozi wa taifa la Tanzania.

Akizungumzia historia ya mashujaa wa vita vya majimaji Kihiyo anasema kuwa  mashujaa  waliozikwa katika eneo hilo walinyongwa na wajerumani  Februari 27 mwaka 1907 na kwamba mashujaa hao walikufa sio kwa sababu ya makosa binafsi bali kwa sababu ya kukataa kuendelea kutawaliwa na wajerumani.

“Licha ya kuwakumbuka mashujaa wa vita vya majimaji,lakini pia tunawakumbuka mashujaa waliokufa katika vita vya pili vya dunia pamoja na askari waliokuwa wanarudi mkoani Ruvuma wakitokea katika vita vya Idd Amini mwaka 1979 ambao walikufa katika milima ya Lukumburu kutokana na ajali hivyo wote wanakumbukwa kama mashujaa wa majimaji”,anasisitiza.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya makumbusho ya Taifa nchini Dk.Constancia Rugumamu  akizungumzia makumbusho ya vita vya Majimaji anasema yanachangamoto nyingi ikiwemo kutafiti historia ya mashujaa na kuboresha tarifa zilizopo na kutafiti zaidi kuhusu mji wa Songea ambao umekuwa ni mji wa kishujaa,kitalii na kihistoria.

Dk.Rugumamu anabainisha zaidi kuwa katika makumbusho ya vita vya Majimaji kutafanyika utafiti na kukusanya taarifa mbalimbali za kambi za wapigania uhuru kusini mwa Afrika zilizokuwepo kusini mwa Tanzania hususani mkoani Ruvuma na kwamba Bodi ya shirika la makumbusho ya Taifa inaona fahari kupewa  jukumu la kuyasimamia makumbusho ya Majimaji.

“Bodi ya shirika la makumbusho ya Taifa ipo katika mchakato wa kuhakikisha kuwa kituo hiki kinakuwa na watalaamu na nyenzo muhimu za uhifadhi wa mikusanyo ya kihistoria na utoaji wa elimu ya makumbusho,pia Bodi inafanya jitihada za kuongeza vivutio vya utalii vilivyomo katika mkoa wa Ruvuma na mikoa ya kusini”,anasema.

Akizungumzia asili  ya majimaji Dk.Rugumamu anasema jina la vita vya majimaji linatokana na imani ya matumizi ya dawa iliyochanganywa na maji,punje za mahindi na mtama zilizosadikiwa kuwa zingempa mpiganaji kinga ya kutodhurika kwa shambulio la risasi za wajerumani.

Vita vya majimaji vilidumu kwa takriban miaka miwili kuanzia mwaka 2005 hadi 2007,waanzilishi wa mwanzo wa vita hivyo walikuwa ni machifu na mganga wa jadi katika jamii ya wangindo na  wamatumbi na baadaye vuguvugu hilo kuenea kwenye jamii nyingi za wamwera,wapogoro,wandendeule,wabena,wangoni,wasangu  na jamii nyingine ambapo Mahenge Songea ilikuwa ni kitovu kikubwa cha mapigano hali liyowalazimu wajerumani kutumia nguvu kuzuia vita hiyo isisambae zaidi.

Kwa muda wa miaka miwili wajerumani walishuhudia waafrika wakiwadhihirishia kwamba dhana waliokuwa nayo kwamba Afrika lilikuwa Bara la giza haikuwa sahihi hivyo iliwalazimu kufanya juhudi kubwa kwa kutumia bunduki,,kuongeza idadi ya wapiganaji na mbinu nyingine za kivita ndipo walishinda vita.

Vita vya majimaji vilikuwa na madhara makubwa kiuchumi na kijamii kwa watu wa mikoa ya kusni mashairiki mwa Tanzania bara ikiwemo kutokea vifo vilivyosababishwa na mapigano,upungufu wa chakula,watu kushindwa kufanyakazi kutokana na kukimbia makazi yao,uchomwaji wa mashamba na maghala ya kuhifadhi chakula uliofanywa na wajerumani na kudhoofisha uwezo wa kushambuliwa.

Wajerumani nao walipata madhara wapiganaji wao waliuawa na wapiganaji wazalendo hivyo vita vya majimaji ni kumbukumbu muhimu katika historia ya Tanzania,mashujaa wa vita vya majimaji wanastahili kuheshimika kwa kuwa walitetea utu,heshima na haki za binadamu,vita vya majimaji ni kielelezo halisi kuwa watanzania walikataa kutawaliwa na wakoloni.

Mwenyekiti wa Bodi ya makumbusho ya Taifa  Dk.Rugumamu anasema orodha ya mashujaa wa majimaji ni kubwa na kwamba majina yote yamehifadhiwa katika orodha ya walionyongwa baada ya kukamatwa na kufungwa na wajerumani wakiwemo machifu wapiganaji Nduna Songea na wenzake.

“Orodha ya mashujaa wa vita vya majimaji inapatikana katika kitabu cha “Historia ya mapambano ya kujikomboa mkoa wa Ruvuma”,vielelezo muhimu vya mashujaa hao vinapatikana katika makumbusho ya majimaji mjini Songea,makumbusho ya majimaji ni tunbu muhimu na rasilimali za utafiti wa historia ya ukombozi wa Tanzania na kivutio cha watalii wa ndani na kutoka mataifa mbalimbali”,anasisitiza.

Hata hivyo Dk.Rugumamu anabainisha zaidi kuwa kumbukumbu za vita vya majimaji pia zinapatikana katika makumbusho ya Azimio la Arusha yaliopo Arusha na makumbusho pamoja na nyumba ya utamaduni iliyopo jijini Dar es salaam.

http://www.maendeleo/ ni vita .blogspot.com







               

No comments:

Post a Comment