Na Albano Midelo
CHUO cha ufundi stadi VETA kilichopo katika Halmashauri ya
manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kinatarajia kujenga mabweni nane ya kulala
wanachuo yatakayogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na mkuu wa chuo hicho
Gideon Ole Lairumbe wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake mjini hapa
Alifafanua kuwa mabweni hayo yatatumika kwa ajili ya kulala
wanachuo wanaotoka mbali na Songea kwa lengo la kuwapunguzia umbali mrefu na
usalama kwa wanachuo wa kike.
Mbali na hilo aliyataja matarajio mengine ya chuo hicho kuwa
ni ujenzi wa ukumbi wa mikutano ,nyumba za watumishi,vyumba vya madarasa na
utengenezaji wa viwanja mbalimbali vya michezo.
Aliongeza kuwa chuo cha VETA kina mpango wa kuanzisha kozi
mpya ya uzalishaji wa chakula yaani food production pamoja na kutoa mafunzo kwa ajili mafundi vinyozi na wasusi wa nywele kwa
akinamama.
VETA Songea imekuwa mstari wa mbele katika kuwajengea uwezo
vijana katika fani mbalimbali ikiwemo
umeme wa majumba, ushonaji, useremala, uungaji vyuma, uashi, ufundi magari, umeme
wa magari, uhadhili na kompyuta kwa wanafunzi wa kozi ndefu jambo ambalo
limepunguza udhururaji na kuepuka vitendo viovu.
Changamoto zinazokikabili chuo hicho kwa mujibu wa mkuu huyo
wa chuo ni pamoja na ukosefu wa sehemu ya kufanyia mazoezi ya vitendo,
na mtazamo hasi kwa
jamii kwamba vijana wanaosoma VETA ni wale walioshindwa kuendelea na elimu ya
juu.
Ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda kuwapokea vijana hao
pindi wanapotafuta ajira na kusisitiza kwa wazazi na walezi kuwapeleka vijana
wao kwenye chuo hicho ili kuongeza ujuzi zaidi.
Kwa mawasiliano albano .midelo@gmail.com

No comments:
Post a Comment