Monday, February 13, 2012

CHAMIWARU yatoa mafunzo ya utawala bora

Pichani kutoshoto washiriki wa mafunzo ya utawala bora wapatao 45 wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo kutoka kwa mwezeshaji Kadili Hamisi kwa ufadhili wa The Foundatio For Civil Society na kuendeshwa na CHAMIWARU.

Na Albano midelo
Chama Cha Michezo kwa Walemavu Ruvuma yaani CHAMIWARU inaendesha mafunzo ya utawala bora  kwa viongozi wa serikali kwenye kata nane za wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.


Mwenyekiti wa CHAMIWARU Namputila Salum alisema mafunzo hayo ambayo yatakuwa yanafanyika kwa siku tano katika maeneo maalum yakishirikisha maofisa ugani,wenyeviti wa vijiji na watendaji wa kata pamoja na wakulima.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo kila eneo litashirikisha washiriki  40 sawa na washiriki 130 katika maeneo ya mafunzo ambayo ni Hanga,Namtumbo na Lusewa wilayani Namtumbo.


Hadi sasa mafunzo hayo yametolewa katika maeneo ya Hanga na Namtumbo na kwamba baada ya mafunzo hayo yatatolewa mafunzo mengine kwa maafisa ugani  wa vijiji kutoka kata nane wapatao 30 .
Mafunzo hayo yanayotolewa na wawezeshaji kutoka jijini Dar es salaam na kufadhiliwa na shirika la The Foundatio For Civil Society  lenye makao makuu yake jijini Dar es salaam ambapo CHAMIWARU imefadhiliwa zaidi ya shilingi milioni 36 kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo.



Kushoto pichani ni washiriki 40 wanaopata mafunzo ya utawala bora  kutoka kata za Suruti na Rwinga wilayani Namtumbo ambao wameanza mafunzo ya siku tano kwenye ukumbi wa parokia ya kanisa katoliki Namtumbo.

No comments:

Post a Comment