Maendeleo ni Vita
Pages
Makala za uchunguzi
Makala za utalii
Makala za Elimu
Makala za mazingira
Makala za kijamii
Habari katika picha
Saturday, March 10, 2012
Ikulu ya Rais wa Msumbiji
Hapa ni eneo muhimu katika historia ya nchi ya Msumbiji.Hapa ni mahali ambapo ni Ikulu ya Rais ambapo kila mwaka Rais anapofanya ziara huwa anafikia hapa eneo la makumbusho ya Taifa .Eneo hili ambalo linaitwa Congresso ndipo kulifanyika mkutano wa mwisho mwaka 1968 ambao ulifanikisha uhuru wa nchi ya Msumbiji mwaka 1975 picha na maelezo na Albano Midelo.
Hapa ni nchini Msumbiji ambako kumejengwa makumbusho ya Taifa.Ukifika kwenye eneo hili utabaini majina ya watu wote walioshiriki kwenye mkutano uliofanikisha uhuru wa nchi ya Msumbiji mwaka 1975.Mkutano huo ulifanyika mwaka 1968.
Hapa napo ni sehemu muhimu katika historia ya Tanzania na Msumbiji.Hili gogo lina historia ya kipekee kwa kuwa mwaka 1968 kwenye gogo hili walifanya mkutano wa mwisho baina ya hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere,hayati Samora Michel na Edward Mondrane ,mkutano huo uliweka mikakati mizito ambayo ilifanikisha uhuru wa Msumbiji ndiyo maana wananchi wa Msumbiji wamehifadhi eneo hili muhimu katika historia ya nchi yao.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment