Christopher
Michael ni daktari wa mimea,binadamu na
wanyama ambaye amesomea nchini Marekani kwa miaka nane, anafanya utafiti wake
wa miaka mitatu mkoani Ruvuma anasema matumizi ya kemikali kama bluekopper kupulizia jirani na vyanzo
vya maji vinasababisha magonjwa zaidi ya
30 kwa binadamu na kwamba tiba ya magonjwa hayo ni gharama kubwa.
Anabainisha
kuwa magonjwa yanayosababishwa na kula au kunywa kemikali au sumu aina ya
bluecopper hayatibiki kwa urahisi ndiyo maana wagonjwa wengi wanaoathirika na
sumu wanaweza kupata matibabu nje ya nchi hususani nchini India kwa gharama
kubwa.
Hata
hivyo amesema mtu ambaye ameathirika na bluecopper anaweza kutambuliwa kwa kati
ya miezi mitatu hadi miaka miwili kutegemea na aina ya ugonjwa aliougua ambapo
ameyataja baadhi ya magonjwa ambayo mtu anaweza kuugua kwa kunywa au kula
kemikali hiyo kuwa ni ugonjwa wa ini,saratani ya damu, figo, ngozi,kuoza sehemu
za siri, kupata mzio, kuoza mapafu, macho,
magonjwa ya kuhara, amiba, kichocho, kuvimba tumbo, ugonjwa wa moyo ambao
humpata mwanamke wakati wa kujifungua.
Kwa
mujibu wa Dk.Michael dalili za mtu ambaye ameathirika na madhara yanayoletwa na matumizi ya bluekopper
ni magonjwa ya ngozi,kung’oka kwa kucha,kuumwa ugonjwa wa macho aina ya trachoma,kope
kuwasha, kupoteza uwezo wa kuona kushindwa kusoma na kuandika,chembechembe hai
za damu kuungua,kuoza mapafu,kiharusi,kuharibika figo, kukosa hewa kwenye
ubongo,kupoteza fahamu na matatizo ya akiri.
“Bluecopper
ikiingia mwilini hakuna dawa za kuweza kuiondoa sumu hiyo ,kinachofanyika
hospitalini ni mtu ambaye anakuwa na dalili kwa mfano za kupoteza fahamu
anapewa dripu la maji ,tatizo la kuathirika na blue copper lipo kila mahali kwenye
vyanzo vya maji vilivyochafuliwa kutokana
na shughuli za kibinadamu, kinachotakiwa ni kutoa elimu ya kutochafua maji
kwenye vyanzo ’’,anasisitiza.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129


No comments:
Post a Comment