Tuesday, March 6, 2012

JET yapata viongozi wake wapya

Na Albano Midelo
CHAMA cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania( JET ) kimejipatia viongozi wake wapya ambao watakiongoza chama hicho katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Viongozi hao wapya wamechakuliwa katika mkutano mkuu wa JET ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa Lion Club jijini hapa na kuhudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote nchini.


Waliochaguliwa ni mwenyekiti mpya wa JET Johson Mbwambo aliyepata kura 44 kati ya kura 48 zilizopigwa ambaye anachukua nafasi ya mwenyekiti mstaafu ambaye ameitumikia JET kwa miaka sita Bw. Deo Mfugale.

Makamu mwenyekiti amechaguliwa kuwa ni Aisha Dachi aliyeshinda kwa kura 47 kati ya 48 zilizopigwa ,katibu mkuu amechaguliwa tena Chrisistoms  Rweimamu ambaye amechaguliwa kwa kura 46 kati ya kura 48.
,Nafasi nyingine ambayo ilikuwa inagombewa kwenye uchaguzi huo ni wajumbe sita ambapo jumla ya wagombea kumi walijitokeza kuwania nafasi hiyo,walioshinda ni Dk.Helen Lotary, Salome Kitomali,Judica Losai,Zainabu Mwachawala, Gerad Kitabu na Ally Haji Amadi.
albano.midelo@gmail.com

No comments:

Post a Comment