MIMI ni mwalimu mstaafu John Joseph Haule ambaye ninaishi
Songea mjini, nilizaliwa Aprili 6,1936,nilikuwa
mwalimu wa shule ya msingi Lupaso,Migongo na Makanya wilayani Masasi
mkoa wa Mtwara katika kipindi cha mwaka 1959 hadi 1966.
Kabla ya kustaafu kazi mwaka1992 nimewahi kufanyakazi katika
wizara ya elimu kama mwalimu katika shule mbalimbali,mratibu elimu,mkuu wa chuo
cha maendeleo ya wananchi na mkaguzi wa shule.
Namba yangu ya pensheni ni 0036642 na TYR 125586.Hata hivyo
pensheni yangu ya Julai hadi Desemba 2011 ambayo ni jumla ya shilingi laki tatu(300,000) haijalipwa kwangu hadi leo
licha ya kuandika barua kadhaa kupitia ofisi ya hazina ndogo mkoa wa Ruvuma
bila mafanikio.
Inadaiwa jina langu linafanana na mstaafu mwingine wa kule
wilayani Mbinga mkoani Ruvuma ambaye anaitwa
John Mhanga Haule hata hivyo namba zetu na sura zetu ni tofauti kabisa.
Mheshimiwa Rais
mstaafu,nikiwa katika shule za wilayani
Masasi wakati huo miongoni mwa washauri wangu wakuu ni pamoja na baba yako
mzazi hayati William Mkapa,padre Philipo Mrope,Kilian Namajojo na Mwenyi John
Mkonona aliyesimamia ubatizo wa mtoto wetu wa kwanza aliyezaliwa katika
zahanati ya Lupaso.
Kwa upendo na heshima uliokuwa nayo kwa wazee wa pale Lupaso
wakiwemo hao ambao nimewataja hapo juu,nakuomba tafadhali unisaidie ili niweze
kupata fedha yangu hiyo kwa kuwa nasumbuliwa mno na magonjwa sugu ya
kisukari,BP,ubovu wa macho na matatizo mengine ya uzeeni.
Sina cha kukupa
,mwenyezi Mungu akubariki ni mimi John Haule wa SLP 128 Songea,simu 0684804290 AU 0714089538.

No comments:
Post a Comment