Na Albano
Midelo
ABATE wa kwanza
mwafrika katika shirika la wabenediktini
la mtakatifu Otilia padre Alcuin Nyirenda ameadhimisha Jubilei ya miaka 25 ya upadre
katika kigango cha Lizaboni parokia ya Songea.
Abate mstaafu
Nyirenda alizaliwa parokia ya Mgazini na kukulia katika kigango cha Lizaboni
ambapo alipata elimu ya msingi katika shule za msingi Ruhuwiko,Mfaranyaki na
Hanga utawani na kupata elimu ya sekondari katika seminari ya Likonde jimbo la
Mbinga.
Abate mstaafu
Nyirenda alipata masomo ya upadre katika seminari kuu za Kibosho na Peramiho na
kupewa daraja takatifu la updare na Askofu mstaafu wa jimbo la Mbinga Emanuel
Mapunda mwaka 1978.
Abate mstaafu
Nyirenda baada ya kupewa daraja la upadre alipewa majukumu mbalimbali yakiwemo
katibu wa utawa wa Abasia ya Hanga,mlezi mkuu wa wanovisi wa Hanga kabla ya
kwenda masomoni Roma nchini Italia
kuanzia mwaka 1991 hadi 1993 kwa ajili
ya masomo ya teolojia ya kitawa katika chuo kikuu cha wabenediktini
wote.
Mara baada ya
kuanzishwa kwa Abasia ya Hanga Desemba 13,1993 padre Alcuin Nyirenda alichaguliwa kuwa Abate wa kwanza mnamo
Januari 15,1994 hivyo kuwa Abate wa kwanza mwafrika katika shirika la
wabenediktini wa mtakatifu Ottilia.
Historia ya Abate
huyo inaonesha kuwa miaka 10 baadaye tangu awe Abate yaani mwaka 2004 alistaafu na kwenda
kufanyakazi makao makuu ya watawa wabenediktini wote ulimwenguni wa kike na wa
kiume huko Roma nchini Italia katika chuo kikuu cha wabenediktini cha mtakatifu
Anselimo ndiko anakoishi na kufanyakazi hadi
sasa.
Akihubiri katika
jubilee hiyo Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Songea mhashamu Norbert Mtega
amepongeza Abate mstaafu Nyirenda kwa kufanikisha kazi ya kichungaji ikiwemo ya
kuwahahasisha waumini wa kigango hicho kujenga kanisa lao la kigango ambalo
hadi sasa limegharimu zaidi ya shilingi milioni 89.
Katika nafasi hiyo
mhashamu Mtega aliwaasa viongozi wa kanisa na serikali kuchukua maamuzi magumu
ambayo ni kusimamia ukweli na kuchukua maamuzi yanayopingana na desturi
zilizozoeleka na watu na inakuwa vigumu kubadilika.
“Maamuzi magumu kwetu
sisi padre ni pale tunapotoa kauli na maamuzi kuhusu maagizo ya mwenyezi
Mungu,kuelezea mambo ya Mungu yanayopingana na desturi zetu kwa mfano kuachana na ushirikina,
uchawi,rushwa,ufisadi na kufuata maagizo ya Mungu inakuwa ni vigumu kwa waumini
kubadilika lakini ni lazima tuchukue maamuzi magumu kutetea
ukweli’’,alisisitiza mhashamu Mtega.
Mhashamu Mtega ametoa
rai kwa waumini na viongozi katika ngazi zote kuchukua maamuzi magumu ili
kuiokoa dunia na Taifa la Mungu na amewaasa mapadre wasifanye kazi kisiasa
badala yake wachukue maamuzi magumu kwa kutetea ukweli pale wanapoona waumini
wao wanaonewa .
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

No comments:
Post a Comment