Thursday, January 24, 2013

TAMH yatoa mafunzo kwa kamati ya utendaji


Viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya TAMH mkoa wa Ruvuma

Na Albano Midelo
VIONGOZI  na wajumbe wa kamati ya utendaji 15 wa  chama  cha watu wenye ulemavu wa akili (TAMH) mkoani Ruvuma wamepata mafunzo ya siku tano ya kuandaa mpango mkakati,usimamizi wa fedha na rasilimali watu.
Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa maktaba mkoa wa Ruvuma yaliofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la The Foundation For Civil Society  yameshilikisha wajumbe kutoka Halmashauri za Songea manispaa,Namtumbo na Songea vijijini.
Mwenyekiti wa TAMH mkoa wa Ruvuma Thadei Mwakaguo alibainisha kuwa shirika la The Foundation For Civil Society limetoa shilingi milioni 7.5 kwa chama hicho kwa lengo la wajumbe wa kamati ya utendaji katika mkoa mzima kuendesha mafunzo ya mpango mkakati ,usimamizi wa fedha  na rasilimali watu.
‘‘Wafadhili baada ya kukubali kutupatia kiasi hicho cha fedha walitoa maelekezo namna ya kutumia fedha hizo ambayo ni kuandaa mpango mkakati wa chama,kuendesha mafunzo ya  usimamizi wa fedha,mafunzo ya katiba kwa wanachama ambao ni wenye ulemavu wa akili na kufanyika mdahalo wa wazi ambao utakusanya mawazo ya wenye ulemavu ambayo yatatumwa katika kamati ya kukusanya maoni ya katiba’’,alisisitiza.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo afisa ustawi wa jamii mkoa wa Ruvuma Anna Mwingira pamoja na mambo mengine aliikumbusha jamii kuachana na mila potofu kuhusu watu wenye ulemavu badala yake sasa kubadilika na kuwashirikisha wenye ulemavu katika mambo mbalim bali kwa kuwa wana nafasi ya kuchangia katika ujenzi wa Taifa.
 Wawezeshaji katika mafunzo hayo  ni Victory Nyenza afisa ustawi wa jamii katika manispaa ya Songea na Mussa Ndomba mkurugenzi  wa shirila lisilo la kiserikali la LESCOTA  ambalo linashughulikia masuala ya watoto waishio katika mazingira hatarishi.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

No comments:

Post a Comment