![]() |
| Mwalimu wa kwanza Tanzania padre John Gama |
Na Albano
Midelo
Mwalimu wa
kwanza Tanzania wa daraja la A(Grade A) ambaye pia alikuwa ni padre wa
jimbo kuu katoliki la Songea padre John Fratera Gama amefariki dunia baada ya
kuugua kwa muda mrefu.
Marehemu padre Gama
amefariki katika hospitali ya misheni Peramiho iliyopo kilometa 24 kutoka mjini
Songea ambako alikuwa amelezwa kutokana na kusumbuliwa na magonjwa ya moyo na
kisukari.
Askofu mkuu wa jimbo
kuu la Songea mhashamu Norbert Mtega amesema kuwa marehemu padri padre Gama
atakumbukwa na watanzania wengi hasa
kutokana na vipaji vyake ikiwemo kuwa miongoni mwa walimu wanne wa kwanza wa
Tanzania waliopewa daraja la daraja A(Grade A) katika chuo cha uliamu Tabora
mwaka 1944.
“ Wananchi wa
kawaida,Mapadre wengi na wahashamu maaskofu kadhaa wa ukanda wa kusini
wamelelewa na kufundishwa naye,amekuwa mwamba wa taaluma hasa katika fani za
falsafa na lugha ya kilatini alioweza kuwafundisha wanafunzi wake kwa umahiri
mkubwa’’,alisisitiza mhashamu Mtega.
Aliongeza kuwa padre
Gama alipenda kujiendeleza kitaaluma na alifarijika kuwawezesha watanzania
wengine kitaaluma kutokana na kuamini kuwa elimu bora ni pato la kuwa na walimu
bora hali ambayo ilileta mafanikio makubwa kiutendaji katika kanisa, taasisi za umma na
watu binafsi
Historia ya maisha
yake inaonyesha kuwa afya yake ilizidi kutetereka kuanzia mwaka 2011 kutokana
na kuzidiwa na tatizo la kisukari ambalo lilidhoofisha mwili wake na
kuathiri mguu wake wa kushoto
uliowalazimisha madaktari kuukata mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu kwa
lengo la kuokoa maisha yake.
Marehemu padre Gama
ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 88 na miaka 56 ya upadre hadi mauti
yanamkuta alikuwa anatoa huduma kama mchungaji na muhudumu wa kiroho katika
hospitali ya mkoa wa Ruvuma ya mjini Songea.
Marehemu padre Gama
alizaliwa Luyangweni wilayani Songea mwaka 1926,elimu ya msingi alipata kati ya
mwaka 1933 hadi 1937 katika shule za msingi Likuyufusi na Mshangano,elimu ya
sekondari kati ya mwaka 1938 hadi 1943 sekondari ya Malangali na mafunzo ya
ualimu aliyapata mwaka 1944 katika chuo cha ualimu Tabora na kutunukiwa cheti
cha ualimu daraja la A.
Masomo ya seminari
aliyapata kati ya mwaka 1945 hadi 1950 seminari za Kigonsera na seminari kuu
Peramiho ambapo chuo kikuu alisoma kati ya mwaka 1965 hadi 1967 Roma Italia
katika chuo kikuu cha Angelicum na kutunukiwa masters ya falsafa.
Padre Gama pia mwaka
1967 hadi 1968 alisoma chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda na kupata
stashahada ya ualimu na mwaka 1977 alisoma chuo cha Chama Cha Mapinduzi
Kivukoni jijini Dar es salaam alitunukiwa stashahada ya siasa ya ujamaa.
Misa ya mazishi ya mwalimu na padre Gama
ilifanyika katika kanisa la kiaskofu la mtakatifu Mathias Kalumba jimbo kuu la
Songea ambayo ilioongozwa na Askofu mkuu Norbert Mtega ambapo mazishi
yaliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Songea yalifanyika katika makaburi ya parokia ya Matogoro nje kidogo ya mji wa
Songea.
albano.midelo@gmail.com

No comments:
Post a Comment