Na Albano Midelo
ZAIDI ya watu 350 wamefariki katika manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma katika kipindi cha kuanzia mwaka 2011 hadi 2012 kutokana
na ugonjwa wa malaria.
Mganga mkuu wa
manispaa ya Songea Dk.Daniel Mtamakaya amesema katika kipindi hicho maambukizo
mapya ya malaria ni zaidi ya 198,492 sawa na asilimia 47 ya wagonjwa waliougua
na kutibiwa matibabu ya nje na kulazwa.
Kutokana na takwimu
za mwaka 2012 pekee zinaonesha kuwa Halmashauri ya manispaa ya Songea ilipokea
jumla ya wagonjwa wa malaria walio na umri chini ya miaka mitano wapatao 41,852
ambao ilikuwa ni sawa na asilimia 48 ya wagonjwa wote waliopokelewa.
Takwimu hizo
zinaonesha kuwa wagonjwa wenye umri
zaidi ya miaka mitano walikuwa ni 51,245 sawa na asilimia 37 ya wagonjwa wote waliopelekwa
na kwamba vifo vilivyosababishwa na malaria kwa watoto chini ya miaka mitano
vilikuwa ni asilimia 65 sawa na asilimia 16 ya vifo vyote.
Dk.Mtamakaya
alibainisha zaidi kuwa vifo vilivyotokea kwa wagonjwa wenye umri zaidi ya miaka
mitano vilikuwa ni 98 sawa na asilimia 15 ya vifo vyote vilivyotokea kwa
wagonjwa wenye umri wa miaka mitano.
Katika kutekeleza
mpango wa Taifa wa ugawaji vyandarua
,jumla ya vyandarua 6831 vimegawiwa katika kipindi cha kuanzia mwaka
2011 na mwaka 2012 kati ya hivyo vyandarua 5188 viligawiwa katika Taasisi na eneo la malazi viligawiwa vyandarua 1643.
Hata hivyo alisema
ili kuhakikisha kuwa mpango wa ugawaji vyandarua unakuwa endelevu,serikali
imeanzisha mpango mpya wa ugawaji vyandarua kupitia wanafunzi wa shule za msingi
na sekondari kwa lengo la kufidia vyandarua vilivyoharibika ambapo mpango huo
unatarajia kuanzia mwaka huu.
Kaimu mkurugenzi wa
manispaa ya Songea Naftari Sailoi ameitaja mikakati ya kupambana na malaria
katika manispaa hiyo kuwa ni pamoja na
kuelimisha jamii kufyeka,kuepuka kulima mazao marefu na kufukia madimbwi
karibu na makazi.
Mikakati mingine aliitaja kuwa ni
elimu kuhusu ukubwa wa tatizo la malaria,dalili zake na jinsi ya kuzuia,kuwahi
matibabu ya malaria,kuzuia maambukizo ya malaria kwa watoto kabla ya kuzaliwa
na kuendelea kutoa vyandarua vyenye dawa kwa wajawazito na watoto.
Waziri mkuu wa Mizengo Pinda akizungumzia hali
halisi ya Ugonjwa wa Malaria alisema Ugonjwa wa Malaria bado unaongoza kuwa
sababu Wagonjwa wengi wanaohudhuria
katika Vituo vya huduma za afya Nchini.
Waziri mkuu Pinda alibainisha kuwa ugonjwa huo
unaongoza kwa kusababisha vifo, hasa kwa Watoto walio chini ya umri wa miaka
Mitano ambapo takwimu kutoka Vituo vya kutolea huduma ya Afya Nchini zinaonesha
kuwa, takriban Wagonjwa Milioni 11 hadi 12 huhudhuria katika Vituo vya huduma
za Afya kwa sababu ya ugonjwa wa Malaria.
Tafiti zilizofanyika katika Jamii Tanzania
HIV/Malaria Indicator Survey (THMIS) katika kipindi cha mwaka 2011/2012
zinaonesha kuwa asilimia 10 ya Watoto katika Kaya wana maambukizi ya vimelea
vya ugonjwa wa Malaria.
Hata hivyo Pinda amezitaja jitihada za Serikali katika kumaliza tatizo la Malaria Nchini ni kuhakikisha Wananchi wanaendelea kujikinga na maambukizi dhidi ya ugonjwa wa huo ambapo Serikali imetekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Mapambano Dhidi ya Ugonjwa wa Malaria wa Miaka Mitano (2008-2013) ambao una lengo la kupunguza vifo kwa Asilimia 80 ifikapo mwaka huu mwishoni.

Hatua nyingine ya
kukabiliana na ugonjwa huo ameitaja kuwa ni usambaza na kuongeza matumizi ya
vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu katika Kaya ambapo hadi sasa zaidi
ya vyandarua Milioni 26 vimesambazwa.
“Serikali tunatekeleza
Mpango wa Hati Punguzo unaolenga kuhakikisha akina Mama Wajawazito na Watoto
wanaozaliwa wanaendelea kupata vyandarua hivyo,
Kuendeleza Mpango wa kunyunyizia dawa ya ukoko majumbani ili kutokomeza mazalia ya Mbu’’,alisisitiza na kuongeza
Kuendeleza Mpango wa kunyunyizia dawa ya ukoko majumbani ili kutokomeza mazalia ya Mbu’’,alisisitiza na kuongeza
Mpango huo unaendelea kutekelezwa katika Mikoa
ya Kagera, Mwanza na Mara ambapo zaidi ya Kaya 1,440,000 sawa na Asilimia 90
katika Wilaya za Mikoa hiyo zitanyunyiziwa viuatilifu. Kutokana na Mpango huo,
zaidi ya Watu 6,500,000 wameendelea kukingwa dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa
Malaria.
Mipango mingine ya kukabiliana na malaria ameitaja kuwa ni Kuendeleza Mpango wa kuangamiza viluwiluwi vya Mbu kwa kutumia njia za Kibaiolojia na kwamba Mpango huo unafanywa na Serikali kwa ushirikiano na Serikali ya Nchi ya Cuba unatekelezwa katika Jiji la Dar es Salaam kuanzia 2011 na kutumia Mwongozo wa kutibu ugonjwa wa Malaria isiyo kali kwa kutumia Dawa ya Mseto ya ALU.

Tangu mwaka 2000 kiwango
cha vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Malaria kimepungua kwa asilimia 25 ambapo
Kuna nchi 50 kati ya nchi 99 zinazoendelea kufanya vyema ili kufikia Malengo ya
Maendeleo ya Millenia kwa mwaka 2015 kwa kupunguza vifo kwa asilimia 75.
Malaria ni ugonjwa
unaoendelea kupukutisha maisha ya watu wapatao 660,000 kila mwaka kutoka kila
kona ya dunia, wengi wao ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaoishi
Kusini mwa Jangwa na Sahara.
Takwimu za shirika la Afya ulimwenguni WHO zinaonyesha kuwa zaidi ya watu millioni 200 wanashambuliwa na ugonjwa wa Malaria na kwamba Kesi nyingi za malaria hazipimwi wala kupatiwa tiba muafaka ambapo dawa zisizo na viwango zinasababisha usugu na kukwamisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.
Kwa mujibu wa WHO idadi vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria hadi kufikia mwaka huu 2013 vimepungua kwa takriban asilimia 20 tu duniani kote katika muongo mmoja uliopita ambapo theluthi moja ya nchi 108 ambazo malaria ilikuwa imeenea zilitarajiwa kutokomeza ugonjwa huo katika kipindi cha miaka 10.

Wataalamu wanasema iwapo malengo
yataendelea kufikiwa, maisha ya watu wengine milioni tatu duniani yanaweza
kuokolewa ifikapo mwaka 2015 na kwamba Malaria ni ugonjwa unaoongoza kwa vifo
duniani ambapo Mwaka 2009, watu 781,000 wamefariki dunia kutokana na malaria.
Ugonjwa huo unaoenezwa na mbu umeenea
zaidi kusini mwa jangwa la Sahara, ambapo asilimia 85 ya vifo vimetokea,ugonjwa
huo umetokomezwa katika nchi tatu tangu mwaka 2007 ambazo ni Morocco,
Turkmenistan na Armenia ambapo Shirika moja la Roll Back Malaria limedhamiria
kutokomeza malaria katika nchi nyingine 10 ifikapo mwisho wa mwaka 2015,
zikiwemo nchi za bara la Ulaya.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

No comments:
Post a Comment