Thursday, October 10, 2013

Mwandata aacha gumzo Zambia


Brighton Mwandata mwanamuziki wa injili TAG Songea
 Na Albano Midelo
MWANAMUZIKI anayeibukia kwa kasi katika muziki wa injili Brighton Mwandata wa mjini Songea baada ya kuzindua albamu yake ya kwanza ya (UTUSAIDIE YESU) ameanza ziara nje ya nchi na mikoa mbalimbali hapa nchini.
Mwandata hivi karibuni ametumbuiza katika mkutano mkubwa wa injili jijini Lusaka nchini Zambia akishirikiana na waimbaji maarufu wa muziki wa injili ambao ni Abiudi Misholi,Daniel Mboya na Martha Baraka.
Wimbo wake wa Nasikia kuitwa aliyoimba kwa lugha ya kabila la Kisafwa la mkoani Mbeya
umewavutia wananchi wengi nchini Zambia ambao waligombania albamu hiyo na kuacha gumzo kubwa katika nchi hiyo.

Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa makala haya Mwandata alisema katika mkutano huo aliweza kuimba nyimbo zake karibu zote za albamu yake ya audio  na video iliyobeba jina la Utusaidie yesu ikiwa na nyimbo nane ilirekodiwa katika studio za Paradise na G&J production mjini hapa kati ya mwezi Machi na Desemba mwaka jana tayari imekamilika .
Mke wa mwanamuziki Mwandata ambaye pia ni mwimbaji
Uzinduzi rasmi wa albamu hiyo ulifanyika katika kanisa la TAG Misufini Songea Julai 21 mwaka huu, mgeni rasmi alikuwa ni mwanasiasa maarufu wa mjini Songea Paulo Mtewele(Mbogolo) ambapo jumla ya shilingi milioni saba zilipatikana.
‘‘Audio na video zimenigharimu karibu shilingi milioni sita,nyimbo zilizopo katika albamu yangu ni simama, usicheze na wokovu, utusaidie Yesu,watashindana,wewe ni baba,nasikia kuitwa na hakuna kama Yesu,katika huduma ya uimbaji hakuna mtu yeyote ambaye ananisaidia iwapo yeyote ameguswa na huduma hii anaweza kunisaidia ilikufikia malengo katika uimbaji’’,alisisitiza.
Mikoa mingine ambayo  amebahatika kutumbuiza na kuitangaza albamu yake ni pamoja na Dar es salaam  Morogoro, Mbeya,Pwani,Dodoma na Njombe na hivi karibuni anatarajia kwenda katika mikoa mingine ya hapa nchini pamoja na nchi ya Kongo DRC.

Mwandata ambaye kitaaluma ni fundi wa vifaa vya umeme alijiingiza katika uimbaji wa nyimbo za injili tangu mwaka 2004 ambapo alijiunga na kwaya ya Soul Winners ya kanisa la TAG Misufini mjini hapa ambayo anaendelea kuimba hadi sasa.
Mwandata  hivi sasa amejiajiri mwenyewe,awali alikuwa anafanyakazi katika shirika la viwanda vidogo SIDO  na kampuni ya Songea Cable Television kabla ya mwaka jana kuacha kazi na kujiajiri yeye mwenyewe  ambapo muda wake mwingi anautumia kwa ajili ya kumtumikia mwenyezi Mungu kwa njia ya uimbaji.
Iwapo unataka kuwasiliana na mwanamuziki huyu unaweza kutumia simu +255753397336 AU +255714917461 BARUAPEPE brighton.mwandata@gmail.com



No comments:

Post a Comment