Rais Jakaya Kikwete amefanya
mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambayo yamewatupa nje mawaziri watano,
kuwaingiza 10 wapya, kuwapandisha manaibu wanne kuwa mawaziri kamili na
kuwahamisha wengine wanane kutoka wizara zao kwenda nyingine.
Miongoni mwa walioachwa katika
mabadiliko
yaliyotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue , ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa ambaye nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji, Dk Binilith Mahenge.
yaliyotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue , ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa ambaye nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji, Dk Binilith Mahenge.
Wengine walioachwa na wizara zao
kwenye mabano ni Manaibu Waziri, Goodlucky Ole Medeye (Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi), Gregory Teu (Viwanda na Biashara), Benedict Ole Nangoro
(Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Philipo Mulugo (Elimu na Mafunzo ya Ufundi).
Mawaziri hao wanaungana na waliokuwa
mawaziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David na
Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais
kutokana na matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya Bunge kuhusu utekelezaji wa
Operesheni Tokomeza Ujangili.
Balozi Sefue alisema kuachwa kwa
mawaziri hao ni moja ya hatua zilizochukuliwa na Rais Kikwete kuimarisha
utendaji serikalini. Pia alisema mabadiliko hayo yametokana na kuwapo kwa
nafasi baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao na kifo cha aliyekuwa
Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.
“Rais amefanya mabadiliko kwa mujibu
wa Ibara ya 55 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa
mamlaka ya kutekeleza wajibu huo,” alisema Balozi Sefue.
Sura mpya
Sura 10 mpya zilizoingia katika
Baraza hilo ni pamoja na Dk Asha Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Katiba
na Sheria, Mbunge wa Busega, Dk Titus Kamani ambaye anakuwa Waziri wa Maendeleo
ya Mifugo na Uvuvi na Naibu wake, Kaika Saning’o ole Telele ambaye ni Mbunge wa
Ngorongoro.
Wengine wapya ni wale walioteuliwa
kuwa Naibu Mawaziri na wizara zao kwenye mabano, Mbunge wa Iramba Mashariki,
Mwigulu Nchemba (Fedha), Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto) na Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama (Elimu na
Mafunzo ya Ufundi).
Pia wapo Mbunge wa Serengeti, Dk
Steven Kwebwe (Afya na Ustawi wa Jamii), Mbunge wa Mbozi Magharibi, Godfrey
Zambi (Kilimo, Chakula na Ushirika), Mbunge wa Mufindi Kusini, Mahmoud Ngimwa
(Maliasili na Utalii) na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo).
Waliopandishwa, kuhamishwa
Mbali na Dk Mahenge, Rais Kikwete
pia amewapandisha manaibu waziri wengine watatu kuwa mawaziri kamili pasipo
kuwahamisha wizara walizokuwa. Hao ni Saada Nkuya Salum anayekuwa Waziri wa
Fedha, Lazaro Nyalandu (Maliasili na Utalii) na Dk Seif Rashid (Afya na Ustawi
wa Jamii).
CHANZO GAZETI LA MWANANCHI

No comments:
Post a Comment