Kila wilaya ya Tanzania kuna aina mbalimbali za madini
Ramani mpya ya madini kutoka
wizara ya nishati na madini inaonesha kuwa kila wilaya hapa nchini inakadiriwa
kuwa na aina 30 za madini.
Maliasili tulizonazo za Madini,gesi na mafuta iwapo hazitasaidia kutatua matatizo na kuboresha huduma za kijamii kama afya,elimu umeme na barabara bora ni sawa na nchi kuwa na laana kwa kuwa rasilimali zilizopo zikisimamiwa kikamilifu zinaweza kuleta maendeleo endelevu kwa watanzania.
Maliasili tulizonazo za Madini,gesi na mafuta iwapo hazitasaidia kutatua matatizo na kuboresha huduma za kijamii kama afya,elimu umeme na barabara bora ni sawa na nchi kuwa na laana kwa kuwa rasilimali zilizopo zikisimamiwa kikamilifu zinaweza kuleta maendeleo endelevu kwa watanzania.
Utafiti umebaini kuwa zipo
sababu mbalimbali zinazoendelea kusababisha madini kushindwa kuwanufaisha
watanzania badala yake madini hayo yameendelea kuwa neema kwa wawekezaji.
Mwanasheria na mkurugenzi wa
chama cha wanasheria watetezi wa mazingira Tanzania(LEAT) Dk.Nshala Rugemeleza
anasema Sekta ya madini inashindwa kuwanufaisha watanzania kutokana na
kumilikiwa na wawekezaji kutoka nje
ambao wanalindwa na sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inafanya
rasilimali ya madini kuendelea kumilikiwa na wageni.
Sheria ya madini ya 2010 ina
vipengele vingi ambavyo vinawabeba wawekezaji kutokana na sheria mpya ya madini
kunukuliwa kutoka mkakati wa Benki ya Dunia
uliodhamiria kuhakikisha kuwa sekta ya madini inaendelea kumilikiwa na
wageni.
Mkakati madhubuti wa Benki
ya Dunia wa mwaka 1992 ulikuwa ni kuhakikisha kuwa nchi za Afrika ikiwemo
Tanzania zinaendelea kupoteza na kushindwa katika soko la dunia kwa madai kuwa
serikali za nchi za Afrika hazina uwezo wa kumiliki mfumo wa uchimbaji madini
badala yake mfumo huo umilikiwe na makampuni binafsi ya nchi za magharibi.
Benki ya Dunia imeweka
msukumo wa kuhakikisha nchi za magharibi zinaendelea kunufaika na sekta ya
madini ya Afrika ambapo benki hiyo ilisimamia na kutoa mkopo wa dola za
kimarekani sh.milioni 50 kwa ajili ya kuifanyia mabadiliko ya sheria ya madini
ya mwaka 1998 na kuanzishwa kwa sheria mpya ya madini ya mwaka 2010.
Hata hivyo katika sheria
hiyo mpya vifungu vingi vimenukuliwa kutoka mapendekezo ya Benki ya Dunia,
mabadiliko ya sheria ya madini ya 2010 haijagusa mabadiliko katika kipengere
cha kodi ili makampuni hayo yaendelee kukwepa kodi ambapo mfumo wa ulipaji kodi
tangu mwaka 1992 hadi sasa bado unawabeba wawekezaji kulingana na mapendekezo
ya Benki ya Dunia.
Mkakati wa Benki ya Dunia
kuhusu madini ya Afrika umeshindwa kutoa jibu la moja kwa moja kwamba madini ya
Afrika yanachimbwa na kuzinufaisha nchi za Afrika badala yake nchi za magharibi
zinaendelea kutafuta vyanzo vipya vya madini ili kuweza kukidhi mahitaji ya
madini katika nchi hizo kwa matumizi ya siku za baadaye.
Kulingana na Benki ya Dunia
sekta ya madini ni ya kilimwengu na kwamba ili iweze kuwa ya kidunia ni lazima
kampuni binafsi za uchimbaji zifanye kazi hiyo kwa kuwa zina mtazamo wa
kiulimwengu katika utafutaji na uchimbaji wake,kampuni hizo zinatoka katika
nchi za Australia, Canada, Afrika ya kusini,Ulaya na Marekani.
Mkakati huo wa Benki ya
Dunia umeeleza wazi kuwa haupo tayari
kuwekeza katika serikali ambayo inachukua Hisa nyingi zaidi ya kampuni binafsi
ambapo watu wenye uwezo mkubwa wa
kifedha ndiyo wanaotakiwa kuwekeza katika sekta ya madini,gesi na mafuta eti
sekta ya madini inahitaji kuwa na mikataba migumu.
Mkakati mwingine wa
kuhakikisha kuwa sekta ya madini inaendelea kuwanufaisha wawekezaji ni
kuhakikisha utafutaji na uchimbaji wa madini unafanyika katika nchi za Afrika
na kusababisha athari za kimazingira ambapo hatua za uchenjuaji, usafirishaji
na utengenezaji wa bidhaa unafanyika katika nchi za wawekezaji ambako wanapata
faida kuwazidi wenye raslimali hizo.
Sekta ya madini inaendelea
kuwanufaisha wawekezaji badala ya wageni ni kutokana na mfumo wa profit Transfering ambao unafanywa
na makampuni ya uchimbaji,mfumo huu unaziwezesha kampuni hizo kufanya biashara
kwa faida kubwa baada ya kuhamishia
faida toka nchi moja yenye kodi kubwa kwenda nchi zenye kodi ndogo.
Kwa mfano kampuni ya BAP
Biliton ya Australia inafanyakazi katika nchi tisa na kusababisha kuongeza
kiwango cha ukilitimba hadi katika kampuni nyingine ndogo ndogo zinazochimba
madini ,mfano mwingine ni kampuni ya Anglo America mwaka 1970 ilimiliki zaidi
ya kampuni 1000 nchini Afrika ya kusini.
Mkakati wa mataifa ya
magharibi kuendelea kumiliki sekta ya madini katika nchi za Afrika walitumia
mbinu mbalimbali ikiwemo mbinu ya kuwa na siri kubwa katika utoaji wa taarifa
ambapo kampuni hizo hazitoi taarifa za kweli kuhusu utafutaji wa madini.----Itaendelea-----
Makala hii imeandikwa na Albano Midelo mwandishi ambaye amesomea masuala ya mazingira,madini,mafuta na gesi.

No comments:
Post a Comment