HALMASHAURI ya
manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ina ziada ya madawati 360 katika shule za
sekondari hadi kufikia Juni 28 mwaka
huu.
Taarifa ya uwepo wa madawati iliyotolewa jana na mkurugenzi wa manispaa hiyo Jenifa Omolo inaonesha kuwa madawati (viti na meza) kwa ajili ya
wanafunzi wa shule za sekondari yamekamilika na kuna ziada ya madawati.
Kwa mujibu wa Omolo
mahitaji ya madawati katika shule za sekondari yalikuwa ni 10,452,yaliokuwepo
ni 9,960,madawati mapya ni 852,yaliopo sasa ni madawati 10,812 na kwamba kuna
ziada ya madawati 360.
Hata hivyo amesema
taarifa ya madawati katika shule za
msingi katika manispaa hiyo zenye jumla
ya wanafunzi 47,348,mahitaji ya madawati
ni 15,783,yaliokuwepo awali ni 9759,yaliotengenezwa ni 5825,madawati yaliopo
hivi sasa ni 15,584 na kuna upungufu wa madawati 199 hadi kufikia Juni 28 mwaka
huu.
“Madawati 199 yanaendelea kutengenezwa katika karakana ya
manispaa ya Songea,yanatarajiwa kukamilika Julai 10,2016’’, imesema taarifa ya
mkurugenzi wa manispaa ya Songea.
Afisa habari wa
manispaa ya Songea Albano Midelo amesema Mradi wa madawati katika manispaa hiyo
ulianza tangu mwezi wa Desemba mwaka 2015
ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
iliyowataka Wakuu wa Mkoa,Wakuu wa
Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha kuwa hakuna wanafunzi wanaokaa chini hadi
kufikia Juni 30 mwaka huu.
Mwisho

No comments:
Post a Comment