Tanzania
inaendelea kupata neema ya rasilimali adimu baada ya Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium imegunduliwa
katika bonde la ufa la Tanzania.
Hadi
sasa Tanzania tayari ina futi za ujazo zaidi ya trilioni 57 za gesi asilia
ambazo zimegunduliwa kwa kiwango kikubwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Watafiti
kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya
Helium nchini Tanzania
hali ambayo inaweza kubadilisha uchumi wa Taifa na kuifanya nchi kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati.
hali ambayo inaweza kubadilisha uchumi wa Taifa na kuifanya nchi kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati.
Kwa mujibu wa ripoti ya idhaa ya Kiswahili
ya BBC ya Juni 28,2016,Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham
kwa ushirikiano na wataalum wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa
takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Katika taarifa kwa wanahabri huko
Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa
umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu
kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika
katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na
teknolojia.
Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa
wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.Mnamo mwaka wa
2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri
kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu huo ulikuwa umesababisha
wataalam kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika
bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi
hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.
''Gesi tuliyoipata huko Tanzania
inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI''
alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.
Mwisho

No comments:
Post a Comment