Msumbiji ina futi za ujazo trilioni 200
Utafiti
ambao umefanywa na mtandao wa www.fikrapevu.com unaonesha kuwa,hali
hiyo inatokana na ukweli kwamba, rasilimali hizo, kama ilivyo kwa madini,
zimeanza kutafutwa na mataifa ya Ulaya tangu
bara hilo likiwa bado linatawaliwa na wakoloni ambao wana utaalamu
kuliko nchi za Afrika.
bara hilo likiwa bado linatawaliwa na wakoloni ambao wana utaalamu
kuliko nchi za Afrika.
Pamoja
na kukosa utaalam ama kuwa na wataalamu wachache, lakini mataifa ya
Afrika
yenye kuzalisha mafuta na gesi yameweka misingi ya kusimamia rasilimali hizo
ikiwemo sheria na kanuni mbalimbali.
Tanzania, kama miongoni mwa nchi zenye rasilimali hizo, nayo imeweka taratibu mbalimbali za kusimamia mafuta na gesi asilia ambayo mpaka sasa imegundulika kiasi cha futi za ujazo trilioni 57.
Tanzania, kama miongoni mwa nchi zenye rasilimali hizo, nayo imeweka taratibu mbalimbali za kusimamia mafuta na gesi asilia ambayo mpaka sasa imegundulika kiasi cha futi za ujazo trilioni 57.
Sheria
hizi karibu zinafanana katika kila nchi ambapo kuna makundi mawili ya sheria
hizo ambapo zipo zilizoandikwa na zipo ambazo hazijaandikwa, lakini zote zikiwa
na malengo ya kulinda rasilimali za taifa.
Sheria
ambazo hazijaandikwa (Unwritten rules) zinahusisha sheria za uzalishaji na
mahitaji (laws of supply and demand), sheria za hatari na ujira (risk and
reward) na sheria za faida na hasara (laws of profit and loss).
Sheria
zilizoandikwa zinahusisha Katiba ya nchi, Sheria za kawaida (statutory laws),
sera, kanuni, na mikataba.
Kuna
uhusiano mkubwa baina ya Katiba, sharia, kanuni na mikataba. Miradi ya mafuta
na gesi asilia inajikita Zaidi kwenye mikataba ambayo inawahusisha washirika
wote kama kampuni za mafuta za taifa (NOC), kampuni za mafuta za kimataifa
(IOC), wakandarasi, wakandarasi wadogo, benki ambazo hutoa mikopo kugharamia
miradi ya utafiti na uzalishaji, kampuni zinazotoa huduma, pamoja na wadau
wengine.
Miongoni
mwa mikataba hiyo, Mkataba wa Serikali Mwenyeji (Host Government Agreement –
HGA au HGC) ndio wa kwanza kabisa, ambao unaiunganisha serikali na kampuni ama
kundi la kampuni.
Mara
nyingi mkataba huo unajulikana kwa majina mengi kama vile; Mkataba wa Mafuta
(Petroleum Contract); Mkataba wa Utafiti na Uzalishaji (Exploration &
Production Agreement – E&P); Mkataba wa Utafiti na Matumizi (Exploration
& Exploitation Contract); Mkataba wa Leseni (License Agreement); Mkataba wa
Uzalishaji wa Pamoja (Petroleum or Production Sharing Agreement – PSA).
mikataba
mbalimbali ya serikali inaweza kugawanywa katika makundi kama Mkataba wa
Maridhiano (Concessional Agreement), Mikataba ya Uzalishaji wa Pamoja
(Production Sharing Contracts), Mikataba ya Huduma (Service Contracts), na
Mikataba ya Ubia (Joint Venture Agreements).
Mkataba
wa Maridhiano ni utaratibu wa maridhiano yanatoa sehemu ya ardhi, na rasilimali
zilizo chini ya ardhi zikijumuishwa, kwa kampuni, ili kama kampuni itagundua
mafuta kwenye kipande cha ardhi, inamiliki mafuta hayo.
Makubaliano
ya Kuchangia Uzalishaji ni uzalishaji wa pamoja baina ya serikali mwenyeji
kupitia kampuni ya taifa inayosimamia mafuta na gesi na kampuni ya kimataifa,
na hayampi mkandarasi umiliki wa mafuta yalioko ardhini; umiliki wa rasilimali
unakuwa kwa dola.
Mkataba
wa Huduma hautoi haki ya kumiliki mafuta ardhini. Katika hali hii kampuni
inalipwa malipo kwa huduma yake katika kuchimba mafuta ya serikali.
Mpangilio
mwingine, ambao mara nyingine huchukuliwa kama ni aina ya nne ya mipangilio ya
kimkataba, ni ubia (Joint Venture), ambao unahusisha dola kupitia kampuni ya
taifa ya mafuta, kuingia ubia na kampuni au kikundi cha kampuni za mafuta. Ubia
wenyewe katika hali hii unapewa haki ya kutafiti, kuendeleza, kuzalisha na
kuuza mafuta.
Kwa
ujumla, mikataba yote hiyo lazima iendane na sheria zilizopo katika nchi husika
ikionyesha utangulizi, tafsiri, haki ya kisheria, mtazamo wa jumla, haki za
msingi, majukumu na wajibu.
Aidha,
mikataba hiyo kwa mujibu wa sheria, inatakiwa kuwa na usiri, kipengele cha
kikomo, kipengele ya kusitisha, kipengele cha kuhusisha usuluhishi ikiwa upande
mmoja utakiuka masharti ama kuona unaonewa, na uwezekano wa kuhamisha kwa
mwingine.
Inafahamika
kwa mafuta au gesi haidumu milele kwa sababu ni rasilimali isiyohuishwa kama
ilivyo kwa madini, hivyo mikataba mingi inaandaliwa kwa kuzingatia uhai wa
mradi wenyewe (life span of a project) tangu kuanza kwake, katikati kwenye
uzalishaji na hadi mwisho kwenye usambazaji.
Maana
yake hapa ni kwamba, lazima kuazingatia vipengele vinne ambavyo ni utafiti,
uendelezaji, uzalishaji, na kuutelekeza wakati uhai wake unapokoma.
Utafiti
unafanyika ili kutambua kama kuna rasilimali husika na taarifa zinazokusanywa
zinapangwa katika makundi 10 tofauti ya mizania ambapo alama sufuri inamaanisha
kwamba hakuna uhakika kabisa; alama 1-3 maana yake ni kwamba hakuna uhakika;
alama 3-5 maara yake hakuna uhakika sana; alama 5-7 maana yake kuna uhakika;
alama 7-9 inamaanisha uhakika mkubwa; na alama 10 maana yake rasilimali hiyo
ipo au imegundulika.
Uendelezaji
wa mradi unafanyika ili kuchimba mafuta mara utafiti unapokuwa umekamilika na
ugunduzi kufanyika ikiwa ni pamoja na kujua kiasi kilichopo, thamani yake na
gharama ya uchimbaji.
Uzalishaji
ni hatua inayofuata baada ya mradi kuendelezwa, maana yake tayari gharama
zinakuwa zimefahamika katika hatua ya uendelezaji, na katika hatua hii ndipo
mafuta au gesi inachimbwa, inasafishwa na kusambazwa katika masoko.
Hatua
ya kutelekeza mradi (abandoning the project) inakuja wakati mradi huo
unapofikia kikomo cha kuzalisha.
--itaendelea
Mtayarishaji wa makala haya ni mwanahabari aliyebobea katika uandishi wa habari za mazingira,gesi na mafuta anapatikana kwa email albano.midelo@gmail.com
No comments:
Post a Comment