kikuu cha mabasi cha Songea kinaendelea kuwa Msamala
Kituo cha mabasi cha
mjini kati ambacho kilizinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwezi Juni mwaka huu
kinatarajiwa kufunguliwa rasmi Julai 29 mwaka huu baada ya kazi ya kukarabati
kukamilika.
Ofisa habari wa manispaa
ya Songea Albano Midelo anasema taarifa ambayo imetolewa na mkurugenzi wa
manispaa ya Songea Tina Sekambo kwa wakuu wa idara na vitengo katika manispaa
hiyo ni kwamba kazi ya kukamilisha ua linalizunguka kituo hicho ipo ukingoni.
Midelo anasema vikao
vya Baraza la madiwani na wataalam wa
manispaa hiyo vilipitisha utaratibu utakaotumika ambapo sasa mabasi makubwa ya
abiria yatakayokuwa yanaingia mjini Songea yanaruhusiwa kuingia katika stendi
hiyo kushusha abiria kwa muda mfupi kisha kurudi kwenye stendi kuu ya mabasi ya
Msamala.
Kwa mujibu wa ofisa habari huyo ukarabati wa Kituo
hicho cha Mabasi ulianza Novemba 25 mwaka 2014 ambapo hatua ya kwanza imehusisha
ujenzi wa eneo la kuegesha na mabasi
uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 499.
Amesema hatua ya pili utahusisha ujenzi wa majengo
ya biashara utakaogharimu kiasi cha
zaidi ya shilingi bilioni 5.25 na
kwamba Majengo hayo ya biashara
yatajengwa na Wafanyabiahara na
wadau mbalimbali kwa njia
ya jenga endesha kabidhi.
Licha ya kukamilika kwa ukarabati wa mradi wa
kituo cha mabasi,mchumi mkuu wa manispaa ya Songea Raphael Kimary amezitaja changamoto
zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi kuwa ni pamoja na kuchelewa kwa
fedha kutoka Wizarani, mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha mvua nyingi
kunyesha hivyo kusababisha
kuchelewa kukamilika Mradi huu kwa wakati.
Baadhi ya wadau wa
usafirishaji mkoani Ruvuma wameunga
mkono ushauri wa wataalam na madiwani wa manispaa ya Songea kuwa kituo kikuu
cha mabasi kinaendelea kubakia Msamala ili kupanua mji na kuongeza mapato
katika manispaa ya Songea.
Pascal Msigwa
mfanyabiashara wa mjini Songea amesema serikali kupitia Baraza la madiwani na
watalaam wameamua uamuzi wa busara kufanya kituo cha mabasi cha zamani kuwa ni
sehemu ambayo mabasi yatakuwa yanashuka
abiria na kurudi kulala Msamala kwa kuwa kituo hicho ni kidogo na hakiwezi
kukidhi idadi kubwa ya mabasi yaliopo mjini Songea hivi sasa.
Mwisho

No comments:
Post a Comment