Tuesday, March 29, 2011

Je unamfahamu binadamu wa kale zaidi duniani



Picha inamuonesha mume wa mgunduzi wa fuvu la binadamu wa kwanza aliyeishi miaka milioni 1.75 iliyopita Dr.Leakey katika eneo ambalo aligundulika binadamu huyo  mkoani Manyara mwaka 1959
Na Albano Midelo

ZAMADAMU (Zinjanthropas) ndiye binadamu wa kwanza wa kale aliyeishi miaka milioni 1.75 iliyopita, aligunduliwa na Dkt. Mary Leakey katika Bonde la Olduvai mkoani Manyara Tanzania Julai 17,1959. Zamadamu huyu ndiye alikuwa wa kwanza kugunduliwa kama ushahidi wa chimbuko la mwanadamu.

Ugunduzi huu ulikuwa wa kipekee na kuifanya Tanzania kujulikana duniani kote kuwa ni sehemu muhimu ya kujifunza historia na maendeleo ya mwanadamu. Mbali ya kugunduliwa kwa Zamadamu wa kale wengi, masalia ya viumbe na zana za mawe pia vilipatikana katika Bonde la Olduvai.

Baada ya Zinjathropas na masalia mengine kugunduliwa yalipelekwa katika Makumbusho ya Taifa la Kenya, Nairobi kwa utafiti zaidi na uhifadhi endelevu ambapo Mwanzoni mwa miaka ya 1960 zilifanyika jitihada za kurudisha baadhi ya mikusanyo nchini Tanzania na mwaka 1965 Zinjathropas alirudishwa nchini na Dr. Leakey na kuikabidhi Serikali ya Tanzania.
Fuvu la binadamu wa kale zaidi duniani ambalo liligunduliwa Tanzania.
Uchunguzi umebaini kuwa Matabaka ya udongo katika Bonde la Olduvai ni mahali pa kipekee ambapo mtafiti wa miamba hawezi kupata shida kujifunza namna na tabia ya maumbile ya ardhi yalivyotokea miaka mingi iliyopita.
http://www.maendeleo/nivita.blogspot.com






























No comments:

Post a Comment