Tuesday, January 18, 2011

Kisiwa kidogo cha puulu kina mengi ya kujivunia katika utalii ziwa Nyasa

kinachoonekana kwa mbali ni kisiwa kidogo cha Puulu kata  ya Liuli  kwenye ziwa Nyasa mkoani Ruvuma ambacho kina utalii wa kihistoria kwa kuwa katika kisiwa hicho wakoloni waliwaweka wagonjwa wa ukoma kati ya mwaka 1910 hadi vita vya kwanza vya dunia,waliwatenga wagonjwa hao kuhofia kuambukiza watu ambao walikuwa hawana ukoma.Hata hivyo mara baada ya uhuru serikali iliamua kuwajengea wagonjwa wa ukoma kambi katika eneo la Ngehe kata ya Kihagara ambao wanaendelea kuishi hadi leo huku wakitunzwa chini ya wizara ya afya na ustawi wa jamii .Kisiwa hicho kina utajiri wa wanyama pori,ndege wa aina mbalimbali pamoja na vitu vingine vingi adimu picha na Albano Midelo

No comments:

Post a Comment