Na Albano Midelo
UNAPOSAFIRI kutoka makao makuu ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea hadi kulifikia jiwe hilo la kihistoria ambalo lipo meta takribani 300 ndani ya ziwa Nyasa inakulazimu kusafiri umbali wa zaidi ya kilometa 200.
Jiwe la Pomonda ambalo wajerumani walilipa jina la sphinxhaven kutokana na kuwa na vivutio lukuki lipo katika historia tangu vita vya kwanza vya dunia mwaka 1914 hadi 1918 pamoja na vita vya pili vya dunia mwaka 1939 hadi 1945 ambapo wakoloni wa kijerumani na waingereza walitumia pango kubwa ambalo lipo kama ukumbi wenye kubeba watu kati ya 60 hadi 100 hivyo wanajeshi wa kiingereza na kijerumani walitumia jiwe hilo kama sehemu ya kujificha wakati wa mapambano.
“Jiwe la Pomonda pia katika kilele chake ambacho kina urefu wa takribani meta 40 kwenda juu ipo taa maalum kubwa yenye rangi nyekundu ambayo ilikuwa itatumiwa na nchi tatu za Tanzania,Malawi na Msumbuji wakati wa wakoloni wa kijerumani,kireno na waingereza kwa ajili ya alama ya kuongozea meli katika ziwa Nyasa ili wasiweze kupotea wanapotaka kutia nanga kwenye bandari ya Liuli,taa hiyo walikuwa wanaweza kuiona hata wakiwa katika nchi za Malawi na Msumbuji.
Vivutio vingine ambavyo vinapatikana kwenye jiwe hilo la kihistoria ndani ya ziwa Nyasa ni kwamba kuna mawe matatu makubwa ambayo wakazi wa eneo hilo wanaamini yamepangwa na mwenyezi Mungu ,huku mpangilio wake ukiwa ni kivutio cha ajabu utadhani yamejengwa na mafundi ujenzi huku yakiwa yameacha njia maalum ambayo unaweza kupita kutokea upande wa pili hali ambayo inawashangaza na kuwavutia wengi.
Jiwe la kihistoria la Pomonda pia ni sehemu muhimu ambayo inafaa kufanya utalii wa kupiga mbizi yaani adventure raping rock kuruka toka juu ya jiwe hadi ziwani umbali wa karibu mita 20 hali ambayo inawavutia watalii wengi kutoka nje ya nchi kwenda mara kwa mara katika jiwe hilo hali ambayo inawafanya wajisikie kana kwamba wapo katika nchi zao ambazo zina maeneo ambayo wameyatengeneza tofauti na eneo hilo la jiwe la Pomonda ambalo ni la asili.
Eneo lote linalozunguka jiwe la Pomonda kupatikana kuna idadi kubwa ya samaki wa mapambo katika eneo ambao inakadiriwa eneo kuna aina zaidi ya 120 wa samaki wa mapambo hivyo mtalii akifika katika jiwe hilo kuna eneo maalumu ambalo anaweza kufanya utalii wa kuvua samaki hao yeye mwenyewe pia anaweza kupika au kupikiwa ugali wa asili wa mhogo ambao ni chakula maalum kwa wakazi wa mwambao mwa ziwa Nyasa.
Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa kuna makampuni ambayo wanaendelea kuwavua samaki hao wa mapambo katika eneo hilo kama shamba la bibi na kwenda kuwauza Ulaya na Marekani kwa bei kubwa huku wenyeji wa kata ya Liuli na maeneo mengine ambako samaki hao wanavuliwa wakibakia mikono mitupu pia serikali inapoteza ushuru halali wa kodi ya samaki hao ambao inakadiriwa wanauzwa ulaya kwa bei ya kati ya shilingi za kitanzania 30,000 hadi 50,000 kwa samaki mmoja.
Jiwe la Pomonda ni eneo ambalo linafaa kwa ajili ya kufanyia picnic kwa kuwa lina ukumbi mkubwa ambao umefunikwa vizuri kwa mawe na mwenyezi Mungu tangu kuumbwa kwa dunia hata wakati wa mvua mtalii anaweza kukaa na kuwa salama,pia kuna eneo maalum ambalo linafaa kwa kupigia picha huku mtalii akipata upepo mwananana wa ziwa Nyasa pamoja na kufanya utalii wa kuzunguka maeneo yote ya jiwe hilo kwa kutumia boti maalum.
Martin Ndomba kutoka kikundi cha Ntembo Tours anashauri watalaamu kutoka wizara ya utalii na maliasili kutembelea katika jiwe la kihistoria la Pomonda ili kufanya utafiti zaidi na kubaini vivutio vingine zaidi na hata umri wa jiwe hilo ambalo linafanana na lile lililopo ziwa Viktoria.
Simu;0766463129
http://www.maendeleo/nivita.blogspot.com
Ahsante sana kwa kunikumbusha kumbukumbu zilikuwa zimeondoka sasa zimerudi tena. Na hongera sana kwa kazi nzuri unayoifanya. Endelea kutuhabarisha.
ReplyDeletePomonda,hakika ni jiwe la kihistoria...Umenikumbusha habari nzuri kwa kijiji chetu cha Liuli..Ubarikiwe kaka kwa kazi nzuri...
ReplyDelete