Mkuu wa brigedi ya kusini mheshimiwa Mhaiki akiweka silaha za jadi kwenye mnara mpya wa mashujaa wa vita vya majimaji nyuma ya ukumbi wa Songea klabu mahali ambapo walinyongwa mashujaa 67 wa vita vya majimaji na wajerumani ambapo mnara huo umejengwa kama sehemu ya kumbukumbu.
Waziri wa maliasili na utalii Ezekiel Maige akipokea ramani ya wilaya 19 za jiji la Lichinga nchini Msumbuji ambayo inaonesha maeneo ya vivutio vya utalii kutoka kwa meya wa jiji la Lichinga Augusto Assifue siku ya kilele cha kumbukizi la vita vya majimaji ndani ya viwanja vya makumbusho ya Taifa ya majimaji.
Jeshi la wananchi wa Tanzania nalo halikuwa nyuma kwenye sherehe za kumbukizi ya mashujaa wa vita vya majimaji hapa wanaingia eneo ambalo umejengwa mnara wa mashujaa.
Aliyeshika microphone ni meya wa jiji la Lichinga nchini Msumbuji Augusto Assifue akiwa na ujumbe wa watu watano wakijitambulisha kwenye viwanja vya makumbusho ya Taifa ya majimaji mjini Songea
No comments:
Post a Comment