Wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia yaani viziwi kutoka shule maalum ya bweni ya mtakatifu Vinsenti ya Ruhuwiko manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakionekana wenye nyuso za furaha baada ya kupokea zawadi kutoka kwa mke wa Rais mama Salma Kikwete ambazo walikabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma.Shule hiyo imekuwa inafanya vizuri kwenye mtihani wa Taifa wa darasa la saba kwa kufaulisha wanafunzi darasa zima karibu kila mwaka.kwa mfano mwaka jana imeongoza katika mkoa wa Ruvuma kwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kufaulisha darasa zima picha na Albano Midelo.
Meneja wa tawi la NMB Songea mkoani Ruvuma akiwa na watoto wenye ulemavu wasioona kutoka shule ya wasioona ya Ruhila manispaa ya Songea ambaye amekuwa akiwafadhili wanafunzi hao katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kuweza kushiriki katika michezo ya wenye ulemavu picha na Albano Midelo
Picha inamuonesha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr.Christine Ishengoma mwenye suti nyeusi alipofika kuitembelea shule ya walemavu viziwi ya mtakatifu Vinsenti ya Ruhuwuko Songea kulia kwake ni mkuu wa shule hiyo Sr.Erenesta Mgayapicha na Albano Midelo
Picha inamuonesha mkuu wa shule ya viziwi ya St.Vinsenti ya Ruhuwiko Songea mkoani Ruvuma Sr.Erenesta Mgaya akimkabidhi mwanafunzi ambaye ni kiziwi na mlemavu wa ngozi yaani albino mafuta maalum ya ngozi ambayo yanamsaidia mlemavu huyo kuepukana na mgonjwa ya saratani ya ngozi ambayo yamekuwa yanawakumba wenye ulemavu wa ngozi kutokana na kushindwa kumudu kununua mafuta hayo ambayo yanauzwa bei mbaya picha na Albano Midelo
No comments:
Post a Comment