Saturday, April 9, 2011

Ijue tovuti ya Maendeleo ni vita

 
Picha inaonesha miongoni mwa fukwe bora na za kuvutia mwambao mwa ziwa Nyasa .Endapo fukwe hizo zilziopo katika eneo la Lundo zinawekezwa kikamilifu inaweza kuwa kivutio kikubwa cha utalii mwambao mwa ziwa Nyasa ambako kuna fukwe niyingi nzuri na za kupendeza.picha na maelezo na Albano Midelo

  Habari za kazi wasomaji wetu wote ambao mnaitembelea tovuti hii ambayo imeanzisha rasmi mwezi Januari 2011,nachukua nafasi hii kuwashukuru wasomaji wote ambao mmekuwa mnaifutilia pamoja na kutoa maoni mbalimbali ili kuboresha tovuti hii ya MAENDELEO NI VITA.
MAENDELEO NI VITA-Taarifa ni Nyenzo kwa muda mfupi ambao imekuwa hewani imeweza kutoa taarifa mbalimbali za mkoa wa Ruvuma,pamoja na taarifa nyingine kutoka mikoa mbalimbali nchini  hali iliyosababisha maelfu ya watu kuitembelea tovuti hii kutoka nchi mbalimbali duniani.
Baadhi ya watu wanaoitembelea tovuti ni kutoka hapa nyumbani Tanzania, Kenya, China, Marekani, Uingereza, Malaysia, Korea, Swedeni, Uholanzi,Ufaransa,Uganda, pamoja na nchi nyingine nyingi.Hata hivyo nachukua nafasi hii kuwatambulisha rasmi MAENDELEO NI VITA nini na imeanzishwa kwa malengo gani.
Miongoni mwa kazi iliyofanywa na KUURU  kuibua vivutia adimu kama fukwe hizi zinazovutia zilizopo katika kata ya Kihagara ziwa Nyasa mkoani Ruvuma ambazo ni kivutio cha utalii
MAENDELEO NI VITA ipo chini ya  Kongano la Urithi na Utalii Ruvuma (KUURU) kwa lugha ya kiingereza ni Ruvuma  Heritage And Tourism Cluster  Initiative (RHTCI).
 KUURU ni mkusanyiko wa watu mbalimbali wenye malengo ya pamoja na wanaofikika kirahisi wakiwemo wanataaluma,wajasiriamali na serikali, ili kupanga mikakati ya kutafuta ufumbuzi na mbinu za kuboresha au kutatua changamoto mbalimbali katika jamii na kuleta mafanikio zaidi.
Lengo la KUURU  ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wanaojihusisha na shughuli za utalii ambao ni wanataaluma,wajasiriamali na serikali  waliopo ndani na nje ya mkoa wa Ruvuma kujishughulisha katika kuibua na kuzitumia rasilimali na malighafi zilizopo ndani ya mkoa wa Ruvuma ili kuharakisha maendeleo ya sekta ya utalii.
Hali hiyo itawezesha kushamiri kwa shughuli za ujasiriamali zenye tija mkoani Ruvuma na hatimaye kuongeza utajiri kwa watu na Taifa kwa ujumla,mkakati wa KUURU unasisitiza kuongeza  utajiri na sio kupunguza umaskini.
Hii ni nyota iliyoanguka katika kijiji cha Ndolezi wilayani Mbozi mkoani Mbeya , KUURU imeweza kwenda kufanya uchunguzi kuhusu nyota hiyo iliyoanguka mwaka 1840 na kuibua changamoto zinazoikabili nyota hiyo pamoja na kuitangaza kwenye vyombo vya habari kutokana na umuhimu wa nyota hiyo katika sekta ya utalii.

KUURU wanaamini kwamba wana Ruvuma wote ni matajiri kwa sababu wanarasilimali za kutosha ambazo iwapo zitatumika vizuri  zitawezesha kuongeza utajiri,kwa maana hiyo sio vizuri kufurahia kupunguza umaskini bali kinachotakiwa ni  kuongeza utajiri kwa kuwa ni vigumu sana kujua umebakiwa na umaskini kiasi gani na utaupunguza na kuumaliza kwa namna gani.
Huu ni mtazamo mpya wa KUURU pia ni changamoto inayoukabili mpango wa kupunguza umaskini  na kukuza uchumi Tanzania MKUKUTA kinachotakiwa hivi sasa ni kuongeza utajiri na kukuza uchumi Tanzania.
Makao makuu ya KUURU ni songea mjini ,KUURU inafanya kazi zake katika wilaya zote za mkoa wa Ruvuma ambazo ni Tunduru,Mbinga,Namtumbo,Nyasa,Songea mjini,Songea vijijini, wakati  mwingine KUURU inafanyakazi nje ya mkoa wa Ruvuma kutegemea mahusiano ya moja kwa moja na shughuli za kongano hili kwa mfano vita vya majimaji,kukutana na wadau na kutembelea vivutio vingine vya utalii.
 Hili ni jiwe la Pomonda,Moja ya vivutio adimu vya utalii ziwa Nyasa ambavyo vimeibuliwa na kutangazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kupitia KUURU
HADI sasa kongano limeanza kufanya tafiti mbalimbali na kuibua vivutio vya utalii ndani ya mkoa wa Ruvuma.vivutio hivyo hutangazwa moja kwa moja kupitia magazeti, majalida ,luninga, tovuti, kutengeneza VCD na DVD, kuandaa vipeperushi vya utalii na kuwaunganisha wajasiriamali kupitia kituo cha kuhatamia wajasiriamali Ruvuma.(Ruvuma interprenuership incubator) ambacho kinaendeshwa na BETTER LIFE TANZANIA.
http://www.maendeleo/ ni vita.blogspot.com

1 comment:

  1. Hakuana siku nimefurahai kama siku ya leo nimekutana na hii mada na hasa kilichonifurahisha kuona hiyo picha ya kwanza nilikuwa nacheza hapo maana ndipo nilipozaliwa.Ahsante sana kwa kunipeleka NYUMBANI KWANGU NILIKOZALIWA.

    ReplyDelete