Thursday, April 28, 2011

Kanisa la TAG Lazindua jimbo jipya la Ruvuma,Fuatilia yaliojili kwenye uzinduzi

Baadhi ya wachungaji wa kanisa la TAG mkoa wa Ruvuma wakifuatilia ibada ya uzinduzi wa jimbo jipya la TAG Ruvuma zilizofanyika katika kanisa la TAG Misufini mjini Songea picha na Albano Midelo.

Picha inamuonesha Askofu mkuu wa kanisa la TAG nchini mhashamu Dk.Barnabas Mtokambali kulia akiwa na katibu mkuu wa TAG  Ron Swai mwenye miwani muda mfupi kabla ya kuanza kwa ibada ya  uzinduzi wa jimbo jipya la TAG Ruvuma ambalo awali lilikuwa katika jimbo la Njombe picha na Albano Midelo.

Picha inamuonesha Askofu mteule wa jimbo la Ruvuma mchungaji Joakimu Mhagama aliyewekewa mikono na maaskofu wengine wa TAG nchini katika kanisa la TAG Msufini mjini Songea ,wakiongozwa na Askofu mkuu wa TAG Dk.Mtokambali picha na maelezo na Albano Midelo.

Askofu mteule wa TAG Ruvuma mchungaji Joakimu Mhagama akikabidhiwa kitabu kitakatifu yaani Biblia kutoka kwa Askofu mkuu wa TAG nchini Dk.Barnabas Mtokambali muda mfupi baada ya kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa kwanza wa TAG katika jimbo la Ruvuma picha na Albano Midelo.

Askofu mkuu wa TAG nchini aliyeshima microphone akiwa pamoja na maaskofu wengine wa TAG nchini wakimsimika rasmi mchungaji Pius Mkinga aliyepiga magoti kuwa makamu wa Askofu wa jimbo la Ruvuma katika hafla zilizofanyika kwenye kanisa la TAG Misufini Songea picha na Albano Midelo.


Askofu mkuu wa TAG nchini Dk.Barnabas Mtokambali akimtangaza rasmi kuwa mchungaji Joakimu Mhagama kuwa ni Askofu kamili wa jimbo la Ruvuma picha na maelezo na Albano Midelo.

Askofu mkuu wa TAG nchini Dk.Barnbas Mtokambali akimtangaza rasmi mchungaji Pius Mkinga kuwa makamu wa Askofu wa TAG jimbo la Ruvuma picha na maelezo na Albano Midelo.

Askofu mkuu wa TAG nchini Tanzania Dk.Barnabas Mtokambali akimtangaza rasmi mchungaji Erasto Luoga kuwa katibu wa  TAG katika jimbo jipya la Ruvuma picha na maelezo na Albano Midelo.

Picha inawaonesha viongozi wa juu wa kanisa la TAG jimbo la Ruvuma wakiwa na wake zao muda mfupi baada ya kusimikwa rasmi na Askofu mkuu wa kanisa hilo nchini.Kutoka kulia ni Makamu wa Askofu mchungaji Pius Mkinga akiwa na mkewe,katikati ni Askofu wa jimbo la Ruvuma mchungaji Joakimu Mhagama akiwa na mkewe na kushoto ni katibu wa jimbo mchungaji Erasto Luoga akiwa na mkewe.

Picha inawaonesha viongozi wateule wa jimbo la Ruvuma mara baada ya kusimikwa rasmi na Askofu mkuu wa TAG nchini ,kutoka kulia mwenye suti nyeusi ni Askofu mkuu wa TAG nchini Dk.Mtokambali,akifuatiwa na makamu wa askofu wa jimbo la Ruvuma mchungaji Pius Mkinga,katikati ni Askofu wa jimbo la Ruvuma mchungaji Joakimu Mhagama na mwisho ni katibu wa jimbo mchungaji Erasto Luoga.
 Picha inamunesha Askofu mteule wa TAG jimbo la Ruvuma mara baada ya kusimikwa akitoa hotuba yake ya kwanza akiwa Askofu kamili kwenye kanisa la TAG Misufini ambako zilifanyika sherehe za uzinduzi wa jimbo hilo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dk.Christine Ishengoma.

No comments:

Post a Comment