Monday, April 25, 2011

Vivutio vya utalii wa michezo ya kupiga mbizi na kuruka jiwe la Pomonda

Hili ndiyo jiwe la kihistoria la Pomonda lililopo mita 300 kutoka Bandari ya Liuli ,moja ya vivutio vinavyopatikana kwenye jiwe hili ni kwamba ukiwa juu ya jiwe hili unaweza kuruka hadi chini ya ziwa umbali wa takribani mita 30 hivyo kuwa ni kivutio cha utalii wa michezo kama utakavyoona katika picha hapa chini picha na maelezo yote kwa hisani ya KUURU na tovuti ya  maendeleo ni vita
Picha zote hapa chini zinaonesha michezo mbalimbali ya  kuruka kutoka jiwe refu la Pomonda lililopo Liuli Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma,eneo hili linafaa sana na linaweza kuwavutia watalii wengi kutokana na kuwa na vivutio lukuki kama unavyoona kwenye picha hizi picha zote kwa hisani ya Maendeleo ni vita.
Picha hii inaonesha hawa watalii wa ndani wakijiandaa kuruka kwenye jiwe la pomonda hadi chini ya ziwa.

Picha hii inaonesha mmoja wa watalii akiruka kuelekea ndani ya ziwa Nyasa umbali wa takribani mita 30.


Hebu mtazame huyu naye akiwa ameruka na kujiandaa kutua ndani ya ziwa Nyasa kutoka katika jiwe refu la pomonda

Mtazame huyu naye inaleta raha, lakini inahitaji kufanya mazoezi ya kutosha .



1 comment:

  1. Haswa inahitajika mazoezi ya kutosha maana duh! Halafu nimekuwa nikijiuliza hivi hakuna mamba humu siku hizi maana nilikuwa mdogo tulikuwa tukiambiwa kuna mamba humo ziwani... Nimejikuta nauliza tu kwa sauti...

    ReplyDelete