Picha inaonyesha Blass Band ya jeshi la magereza mkoa wa Ruvuma ikiongoza maandamano siku ya maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahali pa kazi duniani ambazo kitaifa zimefanyika mkoani Ruvuma ambapo mgeni rasmi alikuwa na waziri wa kazi na ajira Gaudentia Kabaka picha na Albano Midelo.
Wafanyakazi wa kampuni ya Bia Tanzania TBL wakishiriki katika maandamano hayo ambayo yalianzia kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma hadi uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea.
Waziri wa kazi na ajira Gaudentia Kabaka akikabidhi tuzo kwa mwakilishi wa kampuni ya Bia Tanzania TBL Bi.Rose Kailembo,shirika hilo ni miongoni mwa mashirika tisa ambayo yalishinda tuzo na kuwa washindi wa maswala ya afya na usalama mahali pa kazi picha na Albano Midelo.
Natoa hongera kwa sherehe hii, nikizingatia umuhimu wa elimu ya afya na usalama.
ReplyDeleteNaona tangazo la bia hapo juu. Suala la bia ni tata, kwani bia ni chanzo au kichochezi cha ajali nyingi, na uharibifu wa maisha, mali, na afya za wengi. Nimewahi kuandika kidogo kuhusu suala hilo. Soma hapa.