Tuesday, May 3, 2011

Wizara ya maliasili na utalii Ruvuma yang'ara katika maonyesho ya Mei Mosi

Gari la wizara ya maliasili na utalii likiwa lipepambwa na ngozi mbalimbali za wanyama wakiwemo chui,simba,pundamilia pamoja na mafuvu ya wanyama pamoja na wanyama halisi ambao walikuwa wamewekwa kwenye cage siku ya maadhimisho ya sherehe ya wafanyakazi Mei Mosi ambazo kimkoa zilifanyika wilayani Mbinga na mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dk.Christine Ishengoma.Banda la maliasili lilikuwa kivutio cha aina yake hali iliyosababisha watu wengi kumiminika kwenye bando hilo  picha na maelezo na Albano Midelo
Baadhi ya watoto wa shule za msingi wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakiwa katika Banda la maonyesho la wizara ya maliasili na utalii wakishangaa baadhi ya wanyama pamoja na kupata maelezo kuhusu wanyama hao kutoka kwa wataalamu wao walipotembelea kwenye banda hilo picha na maelezo na Albano Midelo.
Gari ambalo lilitumika na wizara ya maliasili na utalii idara ya wanyamapori pamoja na kikosi cha kupambana na ujangili kanda ya kusini kwenye maonyesho ya Mei Mosi ambazo kimkoa zilifanyika kwenye uwanja wa Taifa wa mjini Mbinga,picha na maelezo na Albano Midelo


 Mkuu wa kikosi cha kuzuia ujangili kanda ya kusini Metson Mwakanyamale mwenye suti ya bluu akitoa maelezo kuhusu banda la wizara ya utalii na maliasili kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dk.Christine Ishengoma ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho ya Mei Mosi kimkoa wilayani Mbinga.

Mkuu wa kikosi cha kuzuia ujangili kanda ya kusini Metson Mwakanyamale akiendelea kutoa maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na wizara ya maliasili na utalii kwa watu waliotembelea banda lao la maonyesho  ambalo liliwavutia wengi waliotembelea picha na Albano Midelo.

Waliovutiwa na banda la maonyesho la wizara ya maliasili na utalii sio watu wazima pekee,bali hata vijana na watoto walipenda kufahamu mengi kuhusu maliasili na utalii ambao ndiyo urithi wa Taifa.Hapa Mwakanyamale anaendelea kutoa elimu hiyo kwa vijana kama hawa.

No comments:

Post a Comment