Picha inaonesha jiwe ambalo linaitwa Litembo ambalo pia limezaa jina la kijiji cha Litembo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.Jiwe hilo lilipewa jina hilo na wananchi wa kabila la wamatengo miaka ya 1800 baada ya kulifananisha jiwe hilo na mnyama tembo kama unavyolionaSehemu yenye pango lenye uwazi unaweza kuingia na kutembea ndani kwa ndani kwa dakika 120 na kutokea upande wa pili huku ukishuhudia vivutio vilivyopo ndani ya pango hilo picha na Albano Midelo.
Mwenye kofia ni katibu wa Baraza la mila katika kata ya Litembo Remigius Hyera akitoa historia ya mashujaa wa Litembo ambao walipambana na wajerumani kwa silaha zao duni ambapo mwaka 1902 mashujaa wa kimatengo zaidi ya 800 walipoteza maisha katika eneo hilo baada ya kuuwawa kwa bunduki 19 za wajerumani wakiongozwa na kinara wa wajerumani aliyeitwa jina la Korongo picha na Albano Midelo
Hapa wadau mbalimbali wa utalii mkoani Ruvuma walipotembelea katika kijiji cha Litembo ili kupata historia ya utalii wa kishujaa kutoka katika kabila la wamatengo.Anayetoa maelezo mwenye kofia ni mzee wa mila ambaye kimatengo wanamwita Mpengauturu bwana Alois Ndunguru ambaye alipewa cheo hicho tangu mwaka 1958,kiongozi huyu wa kimila ana uwezo hata wa kuzuia mvua isinyeshe.
Shukrani kwa taarifa na picha hizi nzuri sana. Nilizaliwa na kukulia Litembo, na hii sehemu inayoonekana nimeshatembelea.
ReplyDeleteWanablogu tuna nafasi kubwa ya kuutangaza mkoa wetu na nchi yetu kwa ujumla. Nami nimekuwa na mkakati kama huo wako, na nilishaandika kijimakala kuhusu Litembo. Soma hapa.