Hebu angalia picha hizi halafu toa maoni yako kuhusu hali hiyo hasa mtoto wa kike ambaye amejitosa kusafiri kwa mtindo huu ambao mimi nimeshuhudia live nikiwa nimepanda gari ya nyuma kuelekea Mbambabay wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma picha na Albano Midelo

Picha hii inamuonesha mtoto wa kike sasa amechoka kushikilia nyuma ya gari kwa umbali wa takriban kilometa tisini huku akioga vumbi na upepo mkali,nilipomhoji alisema wamezoea kusafiri kwa mtindo huu ingawa ni hatari sana hasa kwa mtoto wa kike kwa kuwa maumbile yake yanambana.

No comments:
Post a Comment