Monday, June 13, 2011

Jiji la Mwanza kidede kwa usafi nchini Tanzania

Picha ina waonesha baadhi ya watendaji wa jiji la Mwanza  akiwemo mkurugenzi wa jiji Wilson Kabwe wakipokea tuzo kutoka kwa waziri wa makazi profesa Anna Tibaijuka  kwenye hafla ambayo ilifanyika kitaifa kwenye uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea.

  Na Albano Midelo,Songea.
WIZARA ya afya na ustawi wa jamii imelitangaza  jiji la mwanza  kukamata  nafasi ya kwanza katika shindano la afya na usafi wa mazingira  katika Halmashauri za jiji hapa nchini katika kipindi cha  mwaka 2011.

Picha inaonesha mshindi wa jumla wa usafi kitaifa mkoa wa Iringa ambao licha ya kupewa tuzo na zwadi mbalimbali lakini pia walikabidhiwa kombe la ushindi
Mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dk.Daniel Malecela akisoma hotuba ya waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Dk.Hadji Hussein Mponda siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambazo zilifanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea,alisema jiji la Mwanza limeibuka kidedea baada ya kuyashinda majiji ya Dar es salaam  na Mbeya .

Waziri wa afya alilitaja kundi la pili ambalo limeshinda katika shindano la afya na usafi wa mazingira kuwa ni manispaa ya Moshi ambayo imekamata nafasi ya kwanza kati ya Halmashauri za manispaa  17 nchini ambapo manispaa ya  Arusha imeshika nafasi ya pili na  mshindi wa tatu ni manispaa ya Iringa.
 Baadhi ya watumishi wa jiji la Mwanza wakipokea zawadi ya kompyuta kutoka kwa waziri profesa Tibaijuka ambaye alimwakilisha waziri mkuu Mizengo Pinda siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa ilifanyika mkoani Ruvuma.


Mshindi wa kwanza katika nafasi ya Halmashauri za miji nchini kati ya miji sita iliyoshiriki, imechukuliwa na mji wa Mpanda,nafasi ya pili ni mji wa Njombe  ambapo katika Halmashauri 20 za wilaya zilizoshiriki katika shindano hilo ,Halmashauri ya wilaya ya Njombe imekamata nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Halmashauri za Meru na Rungwe.

Aliyevaa sweta ni mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba akipokea tuzo baada ya wilaya hiyo kushinda kwa usafi nchini kati ya Halmashauri 20 

Washindi wote walizawadiwa zawadi zenye thamani tofauti kwa kuzingatia nafasi ya ushindi   na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo waziri wa  ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi profesa Anna Tibaijuka ambaye alimwakilisha waziri mkuu Mizengo Pinda.
       amidelo@yahoo.com

No comments:

Post a Comment