Wilaya mpya ya Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma ni miongoni mwa wilaya mpya nchini.Wilaya hii imemegwa kutoka wilaya ya Mbinga .Wilaya hii inakabiliwa na changamoto niyingi ikiwemo ya usafiri wa kutoaminika hasa wa barabara inayounganisha wilaya hiyo na wilaya za Mbinga na makao makuu ya mkoa wa Ruvuma yaani Songea.Barabara ya nchi kavu inaleta kero kubwa hasa nyakati za masika.hata hivyo wilaya hiyo ina usafiri wa majini kwa kutumia meli ya muda mrefu ya MV Songea kama inavyoonekana hapa imetia nanga katika bandari ya Mbamba-bay ambayo ndiyo makao makuu ya wilaya hiyo.Meli hiyo inaunganisha wilaya hiyo na wilaya za Ludewa iliyopo katika mkoa mpya wa Njombe,wilaya ya Kyela mkoani Mbeya pamoja na nchi jirani ya Malawi picha na maelezo na Albano Midelo
No comments:
Post a Comment