Friday, June 17, 2011

Waandishi wa habari wawili washinda tuzo ya Fellowship kutoka Ruvuma


 Picha inamuonesha  Editha Karlo mwandishi wa New Habari kutoka mkoani Ruvuma ambaye ni miongoni mwa washindi sita wa tuzo ya Fellowship iliowaniwa na waandishi kutoka nchi nzima


Na Mwandishi maalum
WAANDISHI wa habari wawili kutoka mkoani Ruvuma wameibuka miongoni mwa washindi sita  katika  mchuano mkali wa kupata tuzo ya Fellowship inayotolewa na mfuko wa ruzuku kwa vyombo vya habari Tanzania (TMF).

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam  meneja wa TMF  Erenest Sungura  aliwataja washindi hao sita kuwa ni pamoja na  Albano Midelo mwandishi wa kujitegemea kutoka Ruvuma Editha Karlo mwandishi wa New  Habari kutoka mkoa wa Ruvuma,Damasi Kanyabwoya wa The Citzen,Latifa Ganzel wa Uhuru na Mzalendo,Mariam Omary wa Zanzibar Leo na Daniel Mbega wa Mwanasipoti.


Pichani upande wa kushoto inamuonesha Albano Midelo mwandishi wa kujitegemea wa magazeti ya Nipashe na Kiongozi kutoka mkoani Ruvuma ambaye pia ni miongoni mwa washindi sita wa Fellwoship 


Kwa mujibu wa Sungura ushindani wa tuzo hiyo ya Fellwship ulikuwa mkubwa ambapo awali walijitoeza waandishi wengi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ambapo waliofanikiwa kuingi akatika raundi ya pili walikuwa ni waandishi 26 na kwamba washidi hao wamepatikana baada ya jopo la majaji ambao ni wahariri wa vyombo mbalimbali kuwafanyia usaili wa aina kwa ana na kuandika.

Sungura alibanisha zaidi kuwa washindi hao sita  chini ya mpango wa Fellowship  watafanyakazi chini ya wakufunzi waliobobea katika fani za habari kwenye sekta ya kilimo na mazingira ambapo wakufunzi hao watatoka ndani na nje ya nchi.

“Washindi hawa sita wa fellowship watapewa ruzuku ya shilingi milioni mbili kwa mwezi ambazo zitawasaidia katika tafiti zao pamoja na gharama za kuishi katika kipindi chote cha programmu hiyo ambayo itadumu kwa miezi sita,pia watapewa vitendea kazi muhimu vikiwemo kamera ya kisasa,kompyuta(laptop) pamoja na vinasa sauti”,alisisitiza.
 Picha inawaonesha washindi wawili wa Fellowship kutoka mkoani Ruvuma Albano Midelo na Editha Karlo walipokuwa katika chuo kikuu cha Ruaha mjini Iringa anayeonekana kwa pembeni ni mwandishi wa gazeti la Jamboleo mkoani Mbeya Thompson Mpanji

Mpango wa fellowship hufanyika mara moja kwa mwaka ambapo waandishi wanaokuwa wameshinda katika mpango huo  wanajengewa uwezo zaidi na hasa katika eneo maalum ili kuongeza ubora wa  uandishi wa habari za uchunguzi na zile zenye maslahi kwa umma.
Kwa maoni niandikie awamufill@gmail.com







No comments:

Post a Comment