Monday, February 20, 2012

Watano wamaliza kidato cha sita Chipole

Na Albano Midelo

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida shule ya sekondari ya wasichana ya Chipole inayomilikiwa na watawa wa kanisa katoliki jimbo kuu la Songea mkoani Ruvuma mwaka huu wamehitimu wanafunzi watano tu.
Hayo yamebainika kwenye mahafali ya kidato cha sita katika sekondari hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni afisa elimu wa mkoa wa Ruvuma Paulina Mkonongo.
Changamoto nyingine zinazoikabili sekondari hiyo ni pamoja  ukosefu wa walimu wa kutosha,ukosefu wa vitabu vya kiada na ziada na ukosefu wa jengo la kisasa na utawala.



Kulia ni wahitimu wa watano wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana Chipole  wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali  akiwemo mgeni rasmi mwenye taji katikati  Paulina Mkonongo akiwa  na Naibu wa Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Songea  padre Camillus Nikatta.
albano.midelo@gmail.com

1 comment:

  1. Nawapa hongera hao wahitimu. Ni muhimu kuyachukulia matatizo kama changamoto na chachu ya kutufanya tusonge mbele.

    ReplyDelete