Friday, April 27, 2012
Bundi anayedaiwa kukwamisha maendeleo Songea
.Juu ya mnara wa saa kwenye ukumbi huu kuna ndege aina ya bundi ambaye wakati wote amekaa kwenye uwazijuu mnara huu.Baadhi ya wazee maarufu wanadai kuwa bundi huyo ndiye kikwazo cha maendeleo katika mji wa Songea kwa kila wanachodai kuwa anatumika katika imani za kishirikina kuhakikisha kuwa mji huo haupati maendeleo ya kweli.Hakuna ubishi mji wa Songea unakabiliwa na matatizo mengi kwa mfano hadi sasa hakuna umeme wa uhakika na kuaminika hali ambayo inazorotesha uchumi na kufukuza wawekezaji,Songea haina viwanda,maji bado ni tatizo kwa wananchi wengi,huduma nyingi za kijamii bado sio za uhakika hata katika michezo hali ni tete kwa kuwa hakuna timu hata moja inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara tangu iliposhuka daraja timu maarufu ya Majimaji,sio hayo tu nenda ukatembelee stendi kuu ya mabasi mjini Songea utashangaa na hautaamini kama kweli hiyo ndiyo stendi ya mkoa kwa namna ilivyochoka,kuzeeka na kuchakaa.Sasa sijui kama kweli bundi huyu ndiye kikwazo cha maendeleo katika mkoa wa Ruvuma au kuna bundi watu ndiyo wanaokwamisha maendeleo ya mji wa Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla wake?naomba maoni yako
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment