Na Albano
Midelo
MTOTO mwenye maumbile
ya ajabu akiwa na jinsia mbili za kiume na moja ya kike amezaliwa Aprili 25
mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma mjini
Songea.
Mtoto huyo ambaye
bado yupo hai chini ya uangalizi maalum amezaliwa akiwa na hitilafu katika
maumbile yake ikiwa ni pamoja na kuzaliwa na nusu ya ubongo ambayo imetokana na
hitilafu kwenye mfumo wa kichwa hadi uti
wa mgongo.
Muuguzi wa zamu katika wodi ya wazazi katika
hospitali ya mkoa ambako mtoto huyo anaangaliwa Agness Mwinuka amesema mtoto
huyo ambaye amezaliwa na uzito wa kilo moja na gramu 900 amezaliwa akiwa na jinsia mbili za kiume na jinsia moja
ya kike.
“Jinsia moja ya kiume
ipo kama kawaida isipokuwa jinsia moja ya kiume ipo kichwani karibu na kisogo
na jinsia ya kike ipo utosini,mtoto huyu tangu azaliwe juzi hadi sasa hana
uwezo wa kunyonya wala kula kitu chochote ,uchunguzi wa kitabibu bado
unaendelea’’,alisisitiza.
Mama mzazi wa mtoto
huyo Situmahi Mwinuka(32) mkazi wa Msamala mjini Songea anasema huyu ni mtoto
wake wa nne kuzaliwa na kwamba watoto wake wengine watatu hawajawahi kupata
hitilafu yeyote katika mwili.
Kaimu mganga mfawidhi
wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma Dk.Mathayo Chanangula akielezea hali ya mtoto
huyo alisema mtoto anakabiliwa na tatizo ambalo kitaalam ni hitilafu kwenye
mfumo unaoanzia kichwani hadi kwenye uti wa mgongo ambao umesababisha mtoto
huyo kuzaliwa na nusu ya ubongo.
Kulingana na daktari
huyo hitilafu hiyo imesababisha mifumo ya mwili kuwa na dosari ambapo kuna sehemu
mbili za kiume moja ikiwa kichwani na kwamba mtoto anapolia sehemu ya kiume ya
kichwani inasimama na kusisitiza kuwa maisha ya mtoto huyo ni mafupi kutokana
na mifumo ya mwili wake kutokamilika licha ya kwamba mtoto amezaliwa na miezi
tisa.
“Katika nchi
zilizoendelea madaktari bingwa na wenye vifaa vya kisasa wanaweza kuokoa maisha
ya mtoto huyo,hata kama mtoto huyo anaokolewa atakabiliwa na tatizo kubwa la
ulemavu wa akiri kwa kuwa ubongo alionao ni nusu tu ya ubongo unaotakiwa kwa
binadamu kamili’’,alisisitiza.
“Mama anaweza
kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo katika miezi mitatu ya mwanzo
katika ujauzito wake atatumia dawa aina ya flagile,dawa za minyoo,tetesakline
na baadhi ya dawa za malaria kama vile SP ambayo anaruhisiwa kunywa baada ya
wiki 28 na ALU ambayo hairuhusiwi kabisa
kutumika kwa mjamzito kwa ujumla ni marufuku mama mjamzito kunywa dawa bila
kumuona daktari’’,alisisitiza.
Katika hospitali ya
mkoa wa Ruvuma hili ni tukio la kwanza la aina yake mtoto kuzaliwa akiwa na
hitilafu kubwa katika mifumo ya mwili wake.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129
.


No comments:
Post a Comment