Na Albano Midelo
RAIS Jakaya Kikwete mwezi Agosti 2009
alifanya ziara katika mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuangalia shughuli za
kimaendeleo pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.
Siku
ya kwanza ya ziara yake Rais wakati anapita barabarani akitokea uwanja wa
ndege wa Songea wananchi walikuwa wakipiga kelele na kudai umeme huku
wamewasha taa mchana
kutokana na hali halisi ya tatizo sugu la umeme katika mji wa Songea ambalo
lilisababisha mji kuwa giza kutokana na mgawo mkali wa umeme ambao pia
unazorotesha maendeleo ya mkoa wa Ruvuma.
Rais
Kikwete kwa namna ya pekee aliguswa na
alisikitishwa na kasi ndogo ya kushughulikia ufumbuzi wa tatizo la vipuri vya
mashine za kufulia umeme katika mji wa
Songea hali liyosababisha kumwagiza meneja wa TANESCO mkoa wa Ruvuma injinia
Monica Kebara kufuatilia ili kujua vipuli vya mashine hizo vipo wapi na
alitaka kupata ripoti ya vipuri hivyo na mwenendo mzima wa matengenezo
ili wananchi wafahamu kila hatua.
Rais Kikwete hakuishia hapo,badala yake
aliahidi kuileta mashine mpya ya kufua umeme ambayo aliamini ingeweza kumaliza
tatizo la mgawo mkali wa umeme katika mji wa Songea makao makuu ya mkoa wa
Ruvuma hivyo mgawo mkali wa umeme kubakia kuwa historia.
Jambo la kushangaza licha ya mashine mpya ya Rais Kikwete kufungwa na kuanza kutumika kuzalishia umeme katika mji wa Songea ,hali ya umeme katika mji wa Songea tangu mwaka 2009 hadi sasa inazidi kuwa mbaya ambapo maeneo mengi ya mji huo ni giza hadi siku tatu kutokana na mgawo mkali wa umeme unaoendeleo kufanywa na TANESCO.
Matumaini ya Rais Kikwete kuhakikisha kuwa tatizo la umeme katika mji wa Songea litakuwa limemalizika tangu mwaka 2009 yamegonga ukuta ,hali hiyo imewafanya baadhi ya wananchi wa mji wa Songea kupoteza imani na kudai kuwa inawezekana mashine hiyo mpya ilitolewa katika mazingira ya kisiasa zaidi kuliko hali halisi kwa kuwa tatizo la ukosefu wa umeme wa uhakika limeongezeka.
Jambo la kushangaza licha ya mashine mpya ya Rais Kikwete kufungwa na kuanza kutumika kuzalishia umeme katika mji wa Songea ,hali ya umeme katika mji wa Songea tangu mwaka 2009 hadi sasa inazidi kuwa mbaya ambapo maeneo mengi ya mji huo ni giza hadi siku tatu kutokana na mgawo mkali wa umeme unaoendeleo kufanywa na TANESCO.
Matumaini ya Rais Kikwete kuhakikisha kuwa tatizo la umeme katika mji wa Songea litakuwa limemalizika tangu mwaka 2009 yamegonga ukuta ,hali hiyo imewafanya baadhi ya wananchi wa mji wa Songea kupoteza imani na kudai kuwa inawezekana mashine hiyo mpya ilitolewa katika mazingira ya kisiasa zaidi kuliko hali halisi kwa kuwa tatizo la ukosefu wa umeme wa uhakika limeongezeka.
Hamza Chenyewe ni mkazi wa Matarawe mjini
Songea anadai kuwa TANESCO wameshindwa kumaliza tatizo sugu la umeme katika mji
wa Songea na kusisitiza kuwa tatizo la umeme linaonekana kushughulikiwa kisiasa
zaidi na kwamba tatizo la umeme linachangia umasikini kwa wakazi wa Songea
ambao wanashindwa kufanyakazi zao za kiuchumi kutokana na ukosefu wa umeme wa
uhakika.
Chenyewe ambaye ni fundi seremala anasema
ukosefu wa umeme unaleta kero kubwa kwa mafundi ambapo baadhi yao wameshitakiwa
na kufikishwa mahakamani baada ya kushindwa kukamilisha matengenezo ya samani
mbalimbali kwa wakati kutokana na kushindwa kukamilisha kazi za useremela
ambazo haziwezi kufanyika bila umeme .
Adolf Kapinga meneja mstaafu wa kampuni ya
Tanzania motors anasema ukosefu wa umeme wa uhakika umesababisha kuongezeka kwa
ugumu wa maisha unaosababisha mfumko wa bei ambapo hivi sasa kwa mfano bei ya
mchele mjini Songea imepanda kutoka shilingi 1000 hadi 2000 kwa kilo na kwamba
gharama za vyakula kwenye mahoteli au mama lishe pia zimepanda mara dufu.
Agnes Mbonde mkazi wa Lizabon anasema kuwa
ukosefu wa umeme hasa wakati wa usiku unasababisha kuongezeka kwa vibaka ambao
wanapenda giza ili kufanya uharifu na kwamba wanawake ndiyo waathirika wakuu
kutokana na ukosefu wa umeme wa uhakika katika mji wa Songea.
John Mtemi mfanyabiashara wa vifaa vya umeme mjini
Songea anasema ukosefu wa umeme unasababisha biashara yake kuwa ngumu kwa kuwa
wateja wake wanashindwa kujaribu vifaa wanavyokuwa wamevinunua hivyo kuamua
kuacha kununua kuhofia kununua vifaa vibovu ambapo hivi sasa huduma zote na
kila kitu kinachohusiana na umeme
kimepanda bei katika mji wa Songea.
“Wafanyabiashara na watu wenye uwezo wamenunua
jenereta ndogo za kuzalishia umeme,ukipita kwenye mitaa mbalimbali ya mji wa
Songea utaona utitiri wa jenereta,hii ni kutokana na wananchi sasa kukosa imani
tena na umeme wa TANESCO ambao hauaminiki tena wala huwezi kufahamu lina umeme
utawaka na lini utakatika hali ni mbaya’’,anasema Richard Shirima
mfanyabiashara mjini Songea.
Uchunguzi umebaini kuwa ukosefu wa umeme pia
unazorotesha vyombo vya habari vilivyopo mkoani Ruvuma kushindwa kusikilizwa na
kuona na wananchi ambapo baadhi ya redio na luninga sasa ni miezi kadhaa havipo
hewani hali ambayo inawakosesha wananchi haki yao ya kikatiba kupata habari .
Mwanaharakati Mohamed Kudeka mkazi wa Songea
anatoa wito kwa serikali kuachana na umeme wa majenereta ambao matatizo yake
yamekuwa yanajirudiarudia na kusababisha kero kubwa kwa wakazi wa mji wa
Songea.
“Mchawi ni ugonjwa wa majenereta ambayo vipuli
vyake vimechoka na kuchakaa,Rais angeambiwa ukweli kuhusu ukubwa wa tatizo la
umeme angeweza kuleta mashine mpya yenye uwezo mkubwa,tumechoka na kero hii
kama sio ubovu wa mashine utasikia mafuta ya kuendeshea mitambo yamekwisha
TANESCO tuambieni ukweli’’,anasisitiza.
Kaimu
meneja wa TANESCO mkoa wa Ruvuma Haruna Mwachula anadai kuwa ubovu wa mashine
tatu kati ya sita za kuzalishia umeme
katika kituo cha TANESCO mjini Songea mkoani Ruvuma umesababisha mgawo mkali wa
umeme kwa wakazi wa mji huo.
Mwachula
anabainisha kuwa mashine tatu zinazozalisha umeme hivi sasa katika mji wa
Songea zina uwezo wa kuzalisha megawati 2.2
ambapo mahitaji halisi ya umeme katika mji wa Songea ni megawati 4.5 .
“Umeme
unaozalishwa hivi sasa ni karibu nusu ya mahitaji ya umeme katika mji wa Songea
,hali hii imesababisha kuwepo mgawo mkali wa umeme,hata hivyo mashine tatu
ambazo ni mbovu vipuli vyake vimeagizwa na TANESCO makao makuu ‘’,anasema.
Anasisitiza
kuwa mafundi wa TANESCO wanafanyakazi usiku na mchana ambapo tayari
wamefanikiwa kufungua vipuli vyote vibovu kwenye mashine aina ya katapila na ABC
zenye uwezo wa kuzalisha megawati 3.2
Hata
hivyo Mwachula anabainisha kuwa mashine mpya aina ya ABC yenye uwezo wa kuzalisha megawati 1.6
ambayo ilitolewa kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete tayari imefungwa na
inafanyakazi ikisaidiwa na mashine mbili za zamani aina ya wartisila zenye
uwezo wa kuzalisha kilowati 800.
“
Vipuli vipya vikiagizwa na Kazi ya kufunga vipuli katika mashine tatu
ikikamilika itawezesha mashine zote kuzalisha umeme wa megawati 5.5 wakati
mahitaji katika mji wa Songea ni megawati 4.5 hivyo kupatikana kwa umeme wa ziada na tatizo la mgawo wa umeme
kubakia kuwa historia’’,anadai kaimu meneja wa TANESCO mkoa wa Ruvuma.
Hii
ni changamoto kwa TANESCO makao makuu kuhakikisha kuwa vipuli vipya vya mashine za kufulia umeme
vinaagizwa na kuletwa haraka ili kuondoa tatizo hili ambalo hadi sasa bado
halijapata tiba sahihi ambayo ni Songea kuunganishwa kwenye grid ya Taifa au
umeme mbadala wa madini ya makaa ya mawe na uranium ambayo yote yanapatikana
kwa wingi mkoani Ruvuma.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

No comments:
Post a Comment