![]() |
| Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu |
Na Albano
Midelo
OFISI ya mkuu wa mkoa
wa Ruvuma imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya
sh.milioni 2.5 kwa ajili ya kuisaidia timu ya soka ya JKT Mlale iliyofuzu tisa
bora ligi kuu Taifa daraja la kwanza.
Akitoa msaada huo
mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alibainisha vifaa hivyo kuwa ni pamoja
na viatu pea 25 vyenye thamani ya
shilingi milioni 1.5 na mipira 16 yenye thamani y ash.zaidi ya milioni moja.
Akipokea msaada huo
kwa niaba ya mkuu wa kikosi cha jeshi la kujenga Taifa Mlale sajenti Isack
Msaigwa aliishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwa msaada huo ambao
alisema utasaidia kwenye maandalizi ya kushiriki ligi daraja la kwanza Tanzania
bara hatua ya tisa bora.
Naye mwenyekiti wa
chama cha soka mkoa wa Ruvuma Joseph Mapunda alisema kuwa timu ya JKT Mlale
ndiyo timu pekee ambayo inayoweza kuutangaza vema mkoa wa Ruvuma katika soka
baada ya kushuka daraja timu ya Majimaji.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

No comments:
Post a Comment