| Afisa elimu wa mkoa wa Ruvuma Paulina Mkonongo |
Na Albano
Midelo,Songea
WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya wasichana Songea mkoani
Ruvuma wameathirika na sumu inayotolewa
na wadudu waitwao Nairobi flies hali iliyosababisha kutokwa na vidonda
sehemu mbalimbali za mwili.
Risala ya jumuiya ya shule hiyo iliyosomwa katika sherehe ya
mahafali ya 13 ya kidato cha sita ilieleza kuwa
wadudu hao wenye sumu wamekuwa ni
tatizo hasa katika kipindi cha kuanzia mwezi Desemba hadi Mei kila mwaka na
kusababisha vidonda baada ya kutua hasa
sehemu za uso za wanafunzi.
Risala hiyo ilizitaja changamoto nyingine ambazo inawasumbua
wanafunzi hao kuwa ni kuharibika kwa miundo mbinu ya maji safi na maji taka
kutokana na uchakavu,uchakavu wa majengo mbalimbali yakiwemo bwalo la chakula,
mabweni, adarasa,vyoo na madarasa na ukosefu wa maktaba inayokidhi mahitaji ya
kitalaaluma.
Naye mwakilishi wa mkuu wa shule hiyo Weaner Likiliwike alibainisha
shule hiyo kongwe iliyoanzishwa mwaka 1974 yenye wanafunzi wa kidato cha
tano na sita inakabiliwa na ukosefu wa walimu wa masomo ya Sayansi yakiwemo
Biolojia,Kemia na Fizikia.
“Hali ya taaluma katika shule yetu imekuwa ya kupanda na
kushuka ,hii ni kutokana na upungufu wa walimu katika masomo ya
Sayansi,wanafunzi wengi wanaofeli ni
wanaosoma masomo ya Sayansi,pia vifaa katika maabara ni duni’’,alisistiza
Likiliwike.
Jumla ya wanafunzi 295 walipewa vyeti vya kuhitimu kidato cha
sita kwenye mahafali hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa mstahiki meya wa manispaa
ya Songea Charles Mhagama.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129
No comments:
Post a Comment