Na Albano Midelo
CHAMA cha ushirika wa akiba na mikopo cha Ukombozi saccos
kilichopo jimbo kuu katoliki la Songea kimewakopesha wanachama wake 977 mkopo
wenye thamani ya shilingi milioni 552.5 mwaka 2011.
Hayo yalisemwa na
meneja wa saccos hiyo Rainery Ngatunga wakati anasoma taarifa ya chama chake kwenye mkutano mkuu wa nane
uliofanyika kwenye ukumbi wa Centenary mjini hapa.
Alibainisha kuwa mkopo huo ulitolewa kwa wanachama kwa ajili
ya kilimo,mifugo,elimu,afya,ujenzi wa nyumba na biashara na kwamba lengo
lilikuwa kutoa mkopo wa
shilingi milioni 470 katika kipindi cha kuanzia mwezi
Januari hadi Desemba mwaka jana.
Kulingana na meneja huyo hadi
Desemba 31 mwaka jana chama hicho
kilikuwa na Hisa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 26,amana
milioni 43.3 na akiba zaidi ya shilingi
milioni 400.
Naye mwenyekiti wa Ukombozi saccos Gerald Chabruma alisema
saccos hiyo tangu kuanzishwa kwake imepata mafanikio makubwa yakiwemo kutoa mkopo wa zaidi ya shilingi
bilioni moja na kununua gari lenye thamani ya shilingi milioni 15.
Hata hivyo Chabruma ameyataja matarajio ya saccos hiyo mwaka
huu kuwa ni pamoja na kuongeza Hisa kutoka
milioni 26 hadi milioni 32,akiba kutoka milioni 400 hadi milioni 500 na
amana kutoka milioni 43 hadi 50 na
mikopo kutoka milioni 552 hadi 600.
Mgeni rasmi katika mkutano mkuu huo, mama mkubwa wa jamii ya
masista wa mtakatifu Agnes Chipole Sr.Subira Mhowela OSB amewahimiza wanachama
hao kukopa kwa malengo badala ya
kuitumia mikopo hiyo kwa kufanya starehe na anasa.
Ukombozi saccos ambayo ilianzishwa mwaka 2004 ikiwa na
wanachama 49, hivi sasa saccos hiyo idadi ya wanachama imeongezeka hadi kufikia
977.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

No comments:
Post a Comment