HIFADHI za Taifa
Tanzania TANAPA imetoa zawadi ya shilingi milioni
10 kwa waandishi bora wanane wa habari za utalii nchini.
Waandishi hao ni wale
walioshinda tuzo za uandishi bora wa habari Tanzania zilizotolewa na Baraza la
habari Tanzania MCT na kutangazwa rasmi Aprili 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar es salaam mbele ya mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete.
Waandishi hao kutoka
vyombo mbalimbali vya habari nchini walikabidhiwa hundi za fedha zao kati ya
shilingi laki tano hadi milioni moja na nusu na kaimu mkurugenzi mkuu wa TANAPA
Ahmed Mbugi katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa TANAPA mjini Arusha.
Meneja uhusiano wa
TANAPA aliwataja waandishi hao kuwa ni pamoja na Albano Midelo mwandishi wa
habari wa kujitegemea ,Iman Mant gazeti la Dairynews,Juma Nugaz wa Clouds Television na Gordon Kalulunga mwandishi wa kujitegemea.
Aidha TANAPA katika
kuhakikisha kuwa ina watia moyo wanahabari kuandika habari za
utalii,imegharamia safari za kujifunza kwa waandishi hao kwenda nchini Afrika
ya kusini kwa wiki moja lengo likiwa ni kuangalia namna utalii wa ndani
ulivyofanikiwa katika nchi hiyo ambayo ina idadi kubwa ya watalii wa ndani
ukilinganisha na watalii kutoka nje ya nchi.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhi hundi za fedha kwa waandishi hao,kaimu mkurugenzi wa TANAPA
Ahmed Mbugi amesema sekta ya utalii ni muhimu hapa nchini kwa kuwa inachangia
asilimia 17 ya uchumi wa Taifa.
Amewashauri
wanahabari nchini kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili viweze
kufahamika vizuri ndani na nje ya nchi na kwamba wanahabari wanaweza kusaidia
kuiboresha sekta hiyo kutokaka na jamii kuviamini vyombo vya habari hivyo
kusababisha idadi ya watalii kuongezeka mwaka hadi mwaka.
“Nawahakikishieni
TANAPA ipo tayari kushirikiana na wanahabari,tupeni taarifa mapema tunazo
hifadhi za Taifa nyingi ambazo zinavivutio vya aina mbalimbali wakiwemo
wanyama,ndege,mimea na viumbe wengine kwa kutumia kalamu zenu mnaweza
kuwaelimisha wananchi wakatambua umuhimu wa utalii na kutembelea maeneo yenye
vivutio’’,alisema.
Alizitaja hifadhi za
Taifa zilizopo nchini kuwa ni pamoja na hifadhi ya Taifa Arusha, Gombe, Katavi,
Mahale,Mikumi,Ziwa Manyara, Ruaha ,Rubondo,
Serenget,Saadan,Tarangire,Udzungwa,Kitulo,Mkomazi, Saanane na mlima Kilimanjaro.
Wakizungumza mara
baada ya kukabidhiwa hundi zao waandishi hao wameipongeza TANAPA kwa kutambua
mchango mkubwa unaofanywa na waandishi wa habari nchini na kwamba kitendo hicho
kimewapa nguvu ya kujituma zaidi katika kuandika habari za utalii nchini.
albano.midelo@gmail.com

No comments:
Post a Comment