Mishahara pia imeongezwa
MARUPURUPU ya wabunge ikiwamo mishahara imeongezwa kutoka Sh7.4 milioni kwa
mwezi hadi takriban Sh11milioni kwa mwezi, hatua ambayo imeibua mjadala
mwingine mzito miongoni mwao.
Tangu
mwaka jana, wabunge wamekuwa katika vita ya kupokea au kutopokea posho ya
vikao ambayo imekuwa ikikolezwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema),
Zitto Kabwe ambaye alizikataa akisema mbunge anapokuwa kazini hahitaji
kulipwa.
Hata
hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba sasa vita kubwa ipo katika
marupurupu mapya ambayo pamoja na kuchanganya na mshahara yanafikia
Sh11milioni kwa mwezi.
Spika
wa Bunge, Anne Makinda alipoulizwa jana alithibitisha kuhusu kuongezeka kwa
malipo jumla ya wabunge kwa mwezi lakini akasema hafahamu kiwango halisi
kilichoongezwa.
Makinda
alisema nyongeza iliyopo siyo kwa wabunge tu, bali watumishi wote wa Serikali
na ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa
Umma), wakati wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2012/13.
“Hiyo
nyongeza siyo tu kwa wabunge, bali ni kwa watumishi wa Serikali. Tena hiyo
ilitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa
Umma). Sasa ukiniuliza kiasi gani hapo ndipo sielewei, ila najua nyongeza
ipo,” alisema Spika.
Lakini,
vyanzo kutoka ndani ya Bunge vilisema kwamba nyongeza hiyo ambayo tayari
imeingia katika mshahara wa Julai ni Sh3.6milioni, hivyo kufanya jumla ya
fedha anazochukua mbunge kufikia kiasi hicho cha Sh11milioni.
“Hiyo ni vita, kuna wabunge wana hasira kweli hawataki wananchi wajue kama
marupurupu yameongezeka.
Wanaona
wananchi wakijua itakuwa ni tatizo kubwa, watapigiwa kelele lakini nyongeza
hiyo ipo. Tayari wengine wamechukua tangu Ijumaa,” kilisema chanzo kimoja kwa
sharti la kutotajwa jina gazetini.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya wabunge kutoka kundi la
wanaopinga posho kwa wabunge wamepinga pia nyongeza hiyo wakitaka fedha hizo
zielekezwe katika sekta nyingine za kijamii.
Marupuru
ya sasa
Hadi mwezi uliopita, mbunge alikuwa akipokea Sh7.4milioni kwa mwezi ambazo
kati ya hizo Sh2.5milioni ni kwa ajili ya mafuta, Sh2.3 mshahara, Sh170,000
kwa ajili ya mshahara wa dereva, 100,000 kwa ajili ya katibu wa mbunge na
posho ya jimbo.
Hata
hivyo, katika nyongeza hiyo ya sasa haijawekwa wazi kwamba kiasi gani ni kwa
ajili ya mshahara, fedha za mafuta ya gari la mbunge, za dereva, katibu na za
posho ya jimbo na tayari baadhi ya wabunge wameanza kufuatilia mchanganuo wa
nyongeza hiyo.
CHANZO MWANANCHI
        
|
No comments:
Post a Comment