CHUO kikuu Huria cha
Tanzania (OUT) sasa ni cha kimataifa kwa kuwa kina wanafunzi wanaosoma kutoka
nchi mbalimbali za Afrika.
Mmoja wa wahadhiri wa
OUT kutoka makao makuu jijini Dar es salaam Joseph Mbese anazitaja nchi ambazo
wanafunzi wanasoma masomo mbalimbali kutoka OUT kuwa ni pamoja na
Uganda,Rwanda,Kenya na Burundi.
Anabainisha kuwa
wanafunzi hao wanapata masomo yao kwa njia ya mtandao na kwamba wanasoma masomo
yao kupitia mtandao,wanajibu maswali na wahadhili wanasahihisha maswali kwenye
mtandao na kisha mwanafunzi hupata majibu ya maswali na mitihani kwa njia ya
mtandao.
Hata hivyo
anasisitiza kuwa kuanzia mwezi Juni mwaka 2012 masomo yote yamewekwa kwenye
tovuti maalum ya chuo ambapo mwanafunzi anasoma masomo yote na kujibu maswali
kwa njia ya mtandao na kwamba hakuna masomo ambayo yatatumwa kwa njia ya kutuma
vitabu yaani hard copies badala yake masomo yote yatakuwa katika soft copies.
Elimu ya chuo kikuu
Tanzania inaelezeka vizuri zaidi kama historia hiyo itajumuisha sehemu ya
Afrika mashariki ikijumuisha nchi za Tanzania ,Kenya na Uganda.
Baada ya vita kuu ya
kwanza,Afrika mashariki ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza na mkoloni huyo
alikuwa na lengo la kupata asilimia
kubwa ya watu wenye ujuzi na nidhamu ya kazi ndipo alimua kuimarishe
utoaji wa elimu ambapo mwaka 1921
kilianzishwa chuo cha Makerere nchini Uganda kikiwa kinatoa elimu ya
kidato cha nne na kazi ya diploma kwa watu wote wa Afrika mashariki.
Historia ya vyuo
vikuu Afrika mashariki inaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 1949 hakukuwa na chuo
kikuu hadi chuo kikuu cha London nchini Uingereza kilipoamua kukipandisha
hadhi chuo kikuu cha Makerere kuwa chuo kikuu kishiriki cha
chuo kikuu cha London.
Chuo cha Makerere
kiliitwa chuo kikuu cha Afrika mashariki baada ya kupandishwa hadhi ambapo
ilimlazimu mtu yeyote wa Afrika mashariki wakati huo ili aweze kupata elimu ya
chuo kikuu ni lazima kwenda Makerere nchini Uganda ambapo kati ya mwaka 1956 na
1961 kampasi ya Nairobi nchini Kenya na Dar es salaam Nchini Tanzania
zilianzishwa.
Kampasi hizi tatu za
Makerere ziliunda shirikisho la chuo kikuu cha Afrika mashariki mwaka 1963
ambapo kutokana na kushindwa kukidhi mahitaji kampasi hizo zilianzisha vyuo
vikuu ambavyo ni chuo kikuu cha Makerere,chuo kikuu cha Nairobi na chuo kikuu
cha Dar es salaam
Chuo kikuu cha Dar es
salaam kilizunduliwa rasmi na Rais wa awamu ya kwanza hayati Julius Nyerere
Agosti 29,1970 ambapo miaka ya themanini chuo kikuu cha Dares salaam kiliweza
kudahili wanafunzi 900 kwa mwaka wa masomo na baadaye kuanzisha kampasi ya
Morogoro ilianzisha kitivo cha kilimo.
Historia ya vyuo
vikuu nchini inaonesha kuwa kampasi ya Morogoro ilipandishwa hadhi kuwa chuo
kikuu kamili mwaka 1984 na kwamba pamoja na juhudi zote hizo za kupanua elimu
ya chuo kikuu bado mahitaji ya
watanzania kujiunga na vyuo vikuu yalikuwa ni makubwa kuliko uwezo wa vyuo
vikuu.
Hali hiyo ndiyo
iliisukuma serikali kuona uwezekano wa kuanzisha chuo kikuu ambacho kinaweza
kutoa elimu kwa njia ya masafa ndipo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kilianzishwa
chini ya sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992.
Kati ya mwaka 1993
hadi 1994 chuo kikuu Huria cha Tanzania yaani OUT kilipata mkuu wake wa
chuo waziri mkuu mstaafu Dk.John
Malecela na makamu mkuu wa chuo hivi sasa ni professa Tolly Mbwete,udahili
ulianza mwaka 1994 wanachuo wa kwanza walikuwa 766.
Akizungmzia mafanikio
ya OUT tangu mwaka 1992 hadi 2012 mkurugenzi wa OUT kituo cha Ruvuma Andrew
Komba anasema chuo kinakuwa kwa kasi ambapo hadi kufikia mwaka 2011 OUT ilikuwa
imefungua matawi karibu mikoa yote nchini na kwamba Chuo Kikuu Huria
kinatambuliwa kimataifa.
Anabainisha kuwa OUT
ina program 50 za masomo mbalimbali
ambazo zinatolewa Katika ngazi ya cheti,shahada,shahada ya uzamili na shahada ya
uzamivu na kwamba katika kipindi cha
miaka ya 1992 hadi 2012 taasisi za kidini ,mashirika na watu binafsi kuthubutu
kuingia kwenye mchakato wa kutoa elimu ya chuo kikuu bado kuna kazi kubwa .
“Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania kimekuwa msaada mkubwa kwa wanyonge,wasiokuwa na nguvu za
kiuchumi,waliokuwa pembezoni na kutengwa na mifumo mbalimbali,leo hii sio ajabu
hata mfungwa anaweza kusoma ‘’,alisisitiza.
Utafiti ambao
ulifanywa na Benki ya Dunia yaani WB
mwaka 2000 katika baadhi ya nchi za
Afrika, unaonesha kuwa kati ya watu
100,000 wenye sifa na nia ya kupata elimu ya chuo kikuu ni watu 43 tu ndiyo
wanapata fursa hiyo ambapo nchini Afrika ya kusini kati ya watu 100,000 watu1524 wanapata fursa.
Kwa mujibu wa utafiti huo nchini Nambia kila watu
100,000 wenye sifa za kupata elimu ya juu ni watu 738 wanapata elimu ya chuo
kikuu na kwamba utafiti mwingine ambao ambao unafanana na huo uliofanywa hapa
nchini mwaka 2006 unaonesha kuwa kati ya
watu 100,000 watu 129 wanapata fursa ya chuo kikuu.
Takwimu za Tume ya
Vyuo vikuu Tanzania TCU kuhusu udahili wa mwaka 2011/2012 zinaonesha kuwa jumla ya wanachuo 37,924 na kwamba vyuo vikuu,vyuo vikuu vishiriki na taasisi za
elimu ya juu zilizoko nchini hivi sasa zina uwezo wa kudahili wanafunzi 40,000
kwa mwaka.
Kutokana na mchango
mkubwa ambao OUT inatoa kwa elimu ya chuo kikuu Komba anatoa wito kwa
watanzania kutumia fursa ya OUT ambayo inatoa elimu ndani ya mazingira ambayo
mtu anaishi badala ya kusafiri kwenda
mbali kwa lengo la kuitafuta elimu hiyo.
Kwa upande wao
wanachuo wanasoma chuo kikuu Huria cha Tanzania wameishukuru serikali kwa kuanzisha Chuo kikuu
Huria ambapo wamesema hadi sasa idadi kubwa ya watanzania wamefanikiwa kuhitimu shahada mbalimbali na kuongeza ufanisi
katika kazi zao, hivyo kupanda vyeo katika fani na nyadhifa zao.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129
No comments:
Post a Comment