UGONJWA
wa saratani umekuwa tishio katika nchi za Afrika zilizo chini ya Jangwa la
Sahara ikiwamo Tanzania ambapo kwa mwaka 2010, takwimu zinaonesha umeua watu
milioni 9.9 duniani.
Hayo
yalibainishwa na mratibu wa kampeni ya kupambana na ugonjwa huo nchini kutoka
Taasisi ya Tanzania 50 Plus, Mchungaji Dk. Emmanuel Kandusi, alipozungumza na
waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Alisema
saratani ni hatari sana ukilinganisha na takwimu za magonjwa mengine ambapo
malaria uliua watu 500,000, kifua kikuu milioni 2.1, ukimwi milioni 1.8.
Saratani inaongoza kwa kuua watu milioni 9.9.
Alisema
asilimia 75 ya watu waliokufa kwa ugonjwa wa saratani (sawa na milioni 7.4),
walitoka katika nchi zinazoendelea.
Akizungumzia
dalili za saratani ya tezi dume, alisema mgonjwa hupata udhaifu katika
kujisaidia haja ndogo, hisia ya kutaka kupata haja ndogo kila wakati hasa
nyakati za usiku, mkojo kutoka wenyewe, maumivu au kuhisi muwasho wakati wa
haja ndogo na uume kusimama kwa shida.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa jarida la Man, alisema ugonjwa huo unachangiwa na
vyakula vyenye mafuta vikiwemo, nyama, chips mayai, pombe na kutofanya mazoezi ya viungo.
CHANZO TANZANIA DAIMA
|
No comments:
Post a Comment