KATIKA hali isiyokuwa
ya kawaida mwanamke mmoja Jenista Mapunda (24) mkazi wa Mfaranyaki mjini Songea
amejifungua mtoto kisha kumnyonga na kumzika yeye mwenyewe alfajiri ya siku ya
Jumapili katika makaburi ya Mfaranyaki.
Watu waliofika
kushuhudia tukio hilo la aina yake walimshangaa kwa kuwa na roho ya ukatili
hali ambayo pia ilimfanya kuchimba kaburi yeye mwenyewe,kumzika mwanawe na
kuweka msalaba wa mti kama ilivyo desturi kwenye maziko .
Kalista Kifaru(38)
mkazi wa Mfaranyaki alisema majira ya saa 12 alifajiri aliambiwa na mtoto wake
ambaye alipita eneo la makuburi kwamba amemuona mwanamke analia amelala juu ya
kaburi ndipo alitoa taarifa kwa mwenyekiti
wa mtaa wa Mfaranyaki Gabriel Ndewele.
Mwenyekiti wa mtaa wa
Mfaranyaki Gabriel Ndewele akiwa pamoja na baadhi ya wakazi wa Mfaranyaki
walikwenda katika eneo la tukio ambapo walimkuta Jenista akiwa ameishiwa nguvu
kutokana na kutokwa na damu nyingi.
Alipohojiwa Jenista
alidai kuwa kutokana na ugumu wa maisha
alipojifungua karibu na vyoo vya shule ya msingi Misufini aliamua
kumnyonga mtoto wake hadi kufa kisha kumbeba na kwenda kuchimba kaburi na
kumzika kwenye makaburi ya Mfaranyaki.
“Nilipojifungua
niliamua kumnyonga kubeba maiti kuchimba kaburi mimi mwenyewe kisha kumzika, nilizidiwa
pekee yangu niliishiwa nguvu kutokana na kutokwa na damu nyingi,niliamua kulia
na kulala juu ya kaburi la mtoto wangu’’,alisema.
Polisi wamethibitisha
kuwepo kwa tukio hilo ambapo hivi sasa wanamshikiliwa mwanamke huyo kwa upelelezi na uchunguzi
zaidi.Hata hivyo mwanamke huyo amepelekwa kupatiwa matibabu katika hospitali ya
mkoa wa Ruvuma na hali yake inaendelea vizuri.
albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

No comments:
Post a Comment