Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.
Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14,
utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea,
lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga
na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani
mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu
kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna
watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa
kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama
‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni
kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.
Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na
elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya
Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na
kuongeza:
“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini
wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari
kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”
Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni
75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni
0-34.
“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa
kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama
B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo
yake,”alisema Dk Maronga.
CHANZO;GAZETI LA MWANANCHI
No comments:
Post a Comment