Maadhimisho ya sikukuu ya pasaka mwaka huu yameenda sanjari kwa viongozi mbalimbali nchini kutoa maoni na ushauri kwa watanzania kuhusiana na nini kiwe ndani ya katiba mpya ambayo hivi sasa fursa za kutoa maoni zinaendelea kutolewa watu na makundi mbalimbali lengo likiwa kuandika katiba mpya ambayo itakuwa imeshirikisha watanzania wote.
![]() |
| Rais mstaafu Benjamini Mkapa |
Mkapa alisema katiba ijayo haipaswi kuwa na itikadi za kidini kwa kuwa zinaweza kuliangamiza taifa.
“Wapo watakaopata uwakilishi kupitia rasimu ya Katiba ya nchi. Namwomba Mwenyezi Mungu awape mwanga, muhakikishe jambo moja tu ambalo litakuwa msingi mkubwa wa amani na maendeleo na umoja wa taifa letu.
Watupatie Katiba ambayo inatoa fursa kamilifu ya kila mtu kuwa na imani yake.
“Katiba inayoheshimu imani ya kikatiba na imani zote zinazofanywa na wananchi wa Kitanzania…Vilevile ihakikishe kwamba dola au nchi yetu haina imani rasmi kama vile nchi yetu isivyo ya kabila moja, hivyo haiwezekani kuwa na Katiba ambayo inatambua kwa dhana au maandalizi ya vipengele mbalimbali kwamba kuna udini, haiwezekani.”
Askofu na Muungano
Watanzania wametakiwa kuwapuuza watu wanaohubiri kuuvunja Muungano kwani watu hao wana agenda binafsi ambazo si kwa faida au masilahi ya nchi, bali wao na baadhi ya mataifa yanawafanya vibaraka wa kuvuruga amani na utulivu uliodumu kwa miaka mingi.
chanzo ni gazeti la Mwananchi

'Udini' nadharia yenye utata.
ReplyDelete