UGONJWA
hatari unaoshambulia mahindi na kusababisha saratani kwa binadamu umeingia
nchini na wakulima sasa wametahadharishwa kutokula mahindi hayo wala unga ambao
haujakobolewa.
Mahindi
yaliyoathiriwa na ugonjwa huo huota ‘fungus’ ambao ina sumu inayoitwa
‘Aflatoxin’ ambayo inaweza kusababisha madhara kwa wanyama na binadamu hususan
ugonjwa wa saratani.Mbali na kutikisa mikoa kadhaa na kusababisha hasara kubwa
kwa wakulima, ugonjwa huo ambao umeanzia nchini Kenya unaendelea kusambaa kwa
kasi na sasa umeingia pia nchini Uganda.
Awali
ugonjwa huo uliripotiwa kuzikumba wilaya za Babati mkoani Manyara na Meatu
mkoani Shinyanga tu, lakini sasa umesambaa hadi katika mikoa jirani ikiwamo
Kilimanjaro.
Mkuu
wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama jana alilithibitishia gazeti hili kuwa mkoa
wake umekumbwa na ugonjwa huo na tayari umesambaa katika wilaya tatu; Moshi
Vijijini, Siha na Hai. “Ni kweli baadhi ya wilaya zimekumbwa na ugonjwa huo,
bahati mbaya sana hauna tiba na unasambaa kwa kasi... Wataalamu wanaendelea
kuwaelimisha wakulima kutambua dalili zake,” alisema Gama.
Gama
alisema endapo mkulima atabaini shamba lake kushambuliwa na ugonjwa huo katika
hatua za awali, anachotakiwa kufanya ni kung’oa mimea yote ya mahindi na
kuichoma moto.
Mkuu
wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga alisema takriban hekari 14 zimeshambuliwa na
ugonjwa huo katika shamba la Watawa wa Kanisa Katoliki Mailisita na shamba la
mkulima wa Lambo.
Alisema
tayari wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Selian (SARI) ya Jijini
Arusha wamefika wilayani humo na kutoa tahadhari kwa wakulima juu ya athari za
ugonjwa huo. Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, John Bennett anayemiliki
mgahawa wa Golden Shower aliitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi na
wafanyabiashara na kuchukua tahadhari.
“Utajuaje
unga wa dona haukutokana na hayo mahindi au pumba ya chakula cha mifugo
hayakutokana na hayo? Hili jambo ni zito sana si la kufanyia utani hata
kidogo”alisema Bennett.
Mkulima
wa Kijiji cha Kikavu Chini wilayani Hai, Justine Mvungi alisema wataalamu
kutoka SARI wamewataka kuchoma moto miche ya mahindi ambayo watagundua
imeshambuliwa.
“Wametuambia
takriban shamba likishambuliwa, tung’oe mahindi hayo na kuyachoma moto,
wametuambia kama tulishavuna basi tukoboe mahindi hayo maana kiini chake kina madhara,”alisema.“Aliongeza
kusema” hata tukikoboa mahindi tumeambiwa zile pumba zake tusiipe mifugo kwa
sababu itaathirika… Ugonjwa huu wa mmea wa mahindi umeleta taharuki kubwa kwa
wakulima na wananchi.”
CHANZO
GAZETI LA ,MWANANCHI

No comments:
Post a Comment