Saturday, June 15, 2013

Mmiliki wa Blog hii mwandishi bora Tanzania



Na Fransis Godwin,Iringa

Kushoto ni Albano Midelo akikabidhiwa tuzo mbalimbali
  WAZIRI wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki amekabidhi kwa mara ya kwanza tuzo za umahili wa uandishi bora wa habari za uhifadhi zilizoandaliwa na shirika la hifadhi  ya Taifa (TANAPA  2012 TANAPA MEDIS AWARDS


  Aliwataja walioshinda upande wa magazeti kundi la uhifadhi mshindi wa kwanza ni Albano Midelo mwandishi wa kujitegemea wa Nipashe /Kiongozi aliyezawadiwa cheti ,hundi ya Tsh milioni 1.5 ,ngao na safari ya siku saba katika nchi za kusini mwa Afrika kwa kujifunza masuala ya hifadhi, Mussa Juma (Mwananchi) aliyeibuka mshindi wa pili alipata cheti,hundi ya Tsh milioni 1 na watatu ni David Azaria –Habari Leo alizawadiwa cheti na hundi ya Tsh.500,000.   
                         

Mshindi wa kwanza upande wa Radio ni Alex Magwiza -TBC aliyezawadiwa cheti ,ngao ,hundi ya Tsh milioni 1.5 na safari ya siku saba katika nchi za kusini mwa Afrika .


Wakati katika luninga upande wa uhifadhi mshindi wa kwanza alikuwa mshindi mmoja pekee Festo Sikaganamo (ITV) aliyeshinda ngao,hundi ya Tsh milioni 1.5 na safari ya kujifunza utalii nchi za kusini mwa Afrika.


Wakati tuzo ya utalii wa ndani upande wa magazeti mshindi wa tatu ni Elia Mbonea (RAI)cheti na hundi ya Tsh 500,000,mshindi wa pili ni Salome Kitomari (Nipashe) aliyepata cheti na hundi ya Tsh milioni 1 na mshindi wa kwanza alikuwa Phinias Bashaya -Mwananchi aliyeshinda ngao,hundi ya Tsh milioni 1.5 na safari ya kujifunza utalii nchi za SADC.



Eneo la utalii wa ndani vipindi vya radio wa kwanza ni Alex Magweza (TBC) aliyeshinda ngao,hundi ya Tsh milioni 1.5 na safari ya kujifunza utalii nchi za kusini mwa Afrika na wa pili David Rwenyagira (Radio One) aliyepata cheti na hundi ya Tsh milioni moja.


Upande wa utalii wa ndani katika TV mshindi wa tatu ni Juma Nugaz ( Clouds Tv) cheti na hundi ya Tsh 500,000, ,mshindi wa pili ni Raymond Nyamwihula (Star TV) wakati mshindi wa kwanza ni Lilian Shirima (TBC)



Akizungumza baada ya kukabidhi tuzo hizo katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Wiloles HIlltop mjini Iringa waziri Kagasheki alisema kuwa lengo la TANAPA kuanzisha tuzo hizo kwa wanahabari ni kutaka kuona wanahabari wanaandika kwa usahihi na ubora mkubwa habari za uhifadhi ikiwa ni pamoja na kufichua vitendo vya ujangili katika hifadhi hizo .



Waziri Kagasheki amewaasa wanahabari ambao wameshinda tuzo hizo na wale ambao hawakushinda kuendelea kuandika habari za uhifadhi na pale wanapatakiwa kushiriki katika shindano kujitokeza kushindanisha kazi zao.



"Shabaha ya wizara kuanzisha tuzo hizi ni kuwapa moyo wanahabari nchini kote wa kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa ubora ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti mbali mbali"



Hata hivyo amewashauri TANAPA kuendelea kuboresha zaidi tuzo hiyo kama njia ya kuwawezesha wanahabari wengi zaidi kujitokeza ili mwisho wa siku kuweza kuieleza dunia juu ya uhifadhi unaofanywa na Taifa katika uhifadhi kwa kuwa wizara yake inawategemea zaidi wanahabari na vyombo vya habari katika kupambana na vitendo vya ujangili.



 Katika hatua nyingine waziri Kagasheki aliutaja mkakati wa wizara yake ni kuitisha mkutano mkubwa wa wadau wa utalii utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili ya kutafuta njia sahihi ya kudumu katika kutokomeza ujangili wa wanyama katika hifadhi hapa nchini .



Alisema kuwa tatizo la kuuwawa kwa Tembo duniani ni kubwa katika nchi ya Botswana na Tanzania ni ya pili hivyo haitapendeza mikutano mikubwa ya kupambana na ujangili kufanyika nchi za ulaya ambazo hakuna tatizo hilo badala ya nchi husika kama Tanzania.



Pia alisema kuwa mbali ya wizara yake kuanzisha utaratibu huo wa kuwapongeza wanahabari wanaosaidia katika kuhamasisha uhifadhi na kufichua vitendo vya ujangili bado anapongeza jitihada kubwa zinazofanywa na vyombo vya habari nchini katika kukemea vitendo vya ujangili nchini .



Awali meneja Uhusiano wa TANAPA Paschal Shelutete alisema kuwa awali tuzo hizo zilikuwa zikitolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ila kutokana na tathimini waliyoifanya wao wakaona ni vema tuzo hizo kuzitoa katika orodha ya tuzo za MCT na kuzifanya wenyewe TANAPA .



Alisisitiza kuwa lengo la TANAPA ni kuona habari zinazoandikwa zinakuwa na ubora wa hali ya juu na zinaendana na malengo ya Taifa katika uhifadhi hivyo katika mwaka huu ambao ni mwaka wa pili kuzitoa zoezi la kuwapata washindi wa tuzo hizo lilisimamiwa na jaji mkuu Dr.Ayub Rioba pamoja na majaji wengine ambao wamebobea katika tasnia ya habari na masuala ya hifadhi.

Tuzo hizo zilihudhuria na wahariri wa habari kutoka vyombo karibu vyote nchini vya magazeti,radio na televisheni.



 .CHANZO BLOG YA FRANSII GODWIN.





No comments:

Post a Comment