Saturday, July 13, 2013

Mazito yaibuka kuhusu rushwa Tanzania



Dk.Reginald Mengi

  • Vinara wa rushwa nchini wadaiwa kulindwa
  • Vigogo wannewatajwa kuhusika na mtandao 
  • MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, B w. Reginald Mengi, am esema ipo hatari ya Tanzania kuongozwa na viongozi watoa rushwa amba o baadhi yao wapo mahakamani lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yao.Bw. Mengi aliyasema hayo DaresSalaam katika mkut ano wa majadiliano ul ioshirikisha wadau wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TP SF) na Ser ikali.

Alisema kuna watu wanne ambao  ni wakubwa(hakuwataja majina), ambao wan ashindwa kudhibiti vitendo vya rushwa kwa sababu wao ni  wahusika wakubwa katika mtandao huo.


“Hapa Tanzania kuna kitu kinaitwa utashi wa siasa wahusika wanamaanisha kupi ga vita rushwa... jambo hili linafanyika kwa maneno si vitendo kwani asilimia kubwa ya watu wa ngazi za juu ndio wahusika wakubwa wajanga hili.

“Kwa mawazo yangu na maeneo niliyopita, kuna wakubwa wanne hapa nch ini ambao ndio vinara wa mtandao wa rushwa lakini hakuna mtu yeyote anayewataja kutokana na nafasi zao,”alisema Bw.Mengi.

Aliong eza kuwa,asilmia kubwa ya watoaji rushwa ni watu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya nchini na kuwapa vijana ili waziuze hivyo kuhari bu maisha yao na wengine hujikuta wakikamatwa katika nchi mbalimbali.

“Tatizo la rushwa pia lipo kwa viongozi wajuu ambao ndio wahusika wakubwa wa mtandao huu... ni vyema vita ya rushwa na dawa za kulevya ikafanywa kwa vit endo ili kuharakisha maendeleo ya nchi, ”alisema

 CHANZO GAZETI LA MAJIRA


No comments:

Post a Comment